101 views 3 mins 0 comments

TMDA YAZIDI KUWASHIRIKISHA WANANCHI NA WADAU KATIKA KUDHIBITI,UBORA NA USALAMA WA DAWA ILI KULINDA AFYA YA JAMII

In KITAIFA
May 20, 2024

Na Madina Mohammed IRINGA WAMACHINGA

Mamlaka ya dawa na Vifaa Tiba TMDA tangu kuanzishwa kwake Takribani Miaka 21 Sasa,imekuwa ikishirikisha wananchi na wadau Katika Shughuli za udhibiti wa ubora,usalama na ufanisi wa dawa,vifaa na vitendanishi nchini Ili kulinda Afya ya jamii

Hayo ameyasema Leo Tarehe 16 Mei 2024 Katika kikao kazi Cha wahariri wa habari na TMDA Mkuu wa mkoa wa Iringa Peter Serukanga Amesema serikali ya Tanzania Katika jitihada za kuboresha utoaji huduma imekuwa ikishirikisha wadau na wananchi Katika Shughuli zake mbalimbali Ili kufikia matarajio ya jamii Katika sekta ya Afya.

Amesema Moja wapo ya mikakati Katika programu ni pamoja na vikao kazi vya kujadili mikakati mbalimbali ya kulinda Afya ya wananchi.

Aidha Amesema Baadhi ya majukumu ya msingi ya Taasisi ya TMDA ni kuhakikisha Afya ya wananchi inalindwa na kufanya ukaguzi wa mara Kwa mara Ili kuhakikisha kuwa bidhaa zilizopo Katika soko ni salama na zenye ubora.

“Lakini pia Ina jukumu la kudhibiti matangazo ya bidhaa za dawa,na vifaa tiba Ili kuzuia matangazo yenye Nia ya kupotosha umma Kwa lengo la kibiashara”Amesema Serukanga

Pia amebainisha kuwa suala la kudhibiti matangazo ni la kisheria na Katika kuhakikisha utekelezaji wake,zipo kanuni za udhibiti wa matangazo ya dawa na vifaa tiba zilivyoandaliwa chini ya sheria sura 219 na zilianza kutumika tangu mwaka 2010

“Changamoto kubwa ambazo mamlaka imekuwa ikikabiliana nazo Toka kuanzishwa kwake ni kushuhudia kutolewa Kwa matangazo ya bidhaa inazozidhibiti Kupitia vyombo mbalimbali vya habari bila kibali Cha TMDA kinyume na matakwa ya sheria na kanuni na hivyo kuchangia kupotosha jamii”Ameongeza Serukanga

Nae mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Dawa na vifaa tiba TMDA Adam Fimbo Amesema Mamlaka imefanikiwa kuweka na kuimarisha mifumo ya udhibiti wa bidhaa hapa nchini ikiwemo mifumo ya tathimini na usajili wa bidhaa,ukaguzi wa viwanda na maeneo ya biashara,utoaji na uingizaji bidhaa,ufuatiliaji wa usalama wa dawa pamoja na majaribio ya dawa

“TMDA Katika utekelezaji wa majukumu yake inafanya chunguzi za kiimaabara Ili kufanya maamuzi ya kisayansi Katika kujiridhisha ubora,usalama na ufanisi wa bidhaa”.Amesema Fimbo

Fimbo amebainisha kuwa mamlaka imewekeza vya kutosha Katika maabara Kwa kuweka vifaa vya kisasa na mafunzo ya wataalamu

Aidha uwekezaji umeifanya maabara ya TMDA kuwa maabara inayoaminiwa na kutumika kama maabara rejea barani Afrika pia maabara ya dawa imepata ithibati na upimaji wa vifaa tiba na vitendanishi imepata ithibati Katika njia za wananchi Kwa kuwa matokeo ya udhibiti yanakubalika Duniani na kuondoa hofu Katika ubora.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram