Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH Dr AMOS NUNGU amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi ya kukuza bunifu za kisayansi na teknolojia kwa vijana hivyo kuwahimiza vijana kuendelea kuwasilisha bunifu zao ili ziendelezwe na kuleta tija kwa taifa
Akizungumza hii leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kielekea wiki ya bunifu nchini, amesema budget ya kuendeleza bunifu za Kisayansi zipo na kuwahimiza vijana kuja na bunifu ambazo zinahitajika sokoni na zitakuwa na faida kubwa kwao na jamii kwaujumla
“Kumekuwa na utikio mkubwa wa ubunifu Kuna Vijana wengi wanakuja na ubunifu zao lakini pia tumesema serikali imeeka mazingira wezeshi la jukwaa la Vijana kujitokeza kuonyesha ubunifu zao Sasa hizi bunifu Kuna bunifu zengine hazipo kufikia maji teyali”
“tuendelee kuwahimiza Vijana walete bunifu zao na serikali inatoa huo usaidizi kadri wa mahitaji yanayoitajika Katika ubunifu lakini kikubwa Katika uzoefu wetu ni kitu Cha mwisho”.Amesema Nongwe
Aidha Nongwe Nongwe Amesema kuwa mitaji IPO Kwa kama Kuna Vijana wanabunifu na wamekosa mitaji na mitaji IPO na changamoto IPO baadhi ya bunifu nyingi hazina mlaji zinapendeza kuangalia na kuziona Kwa macho lakini mlaji hayupo
Nae mkurugenzi idara ya sayansi Teknolojia na Ubunifu wizara ya Elimu sayansi na Teknolojia Ladislaus Mjune Amesema Kupitia mtaala wetu mpya walimu wanaitajika kutoa elimu na wanaendelea kupata mafunzo Zaidi Ili Zaidi ya kuwafundisha Vijana wawe pia na uwezo wa kubaini vipaji maalum kutoka Katika Vijana wanaowafundisha
“Kupitia tume yetu ya sayansi na Teknolojia Kuna utaratibu wa mashindano ya taifa ya Teknolojia na Ubunifu na utaratibu huo unatusaidia tuweze kubaini Teknolojia na bunifu mbalimbali kutoka kila nchi ya Taifa letu”Amesema Mjune