298 views 33 secs 0 comments

WAZIRI KASSIM MAJALIWA KUWA MGENI RASMI KONGAMANO LA JUMIKITA

In KITAIFA
May 18, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

Jumuiya ya mitandao ya kijamii Tanzania JUMIKITA Kwa kushirikiana na TAHLISO wameandaa kongamano la wanahabari wa mitandao ya kijamii nchini litakalofanyika tarehe 20 Mei 2024 Katika ukumbi wa maktaba ya chuo kikuu Cha Dar es salaam”

Hayo ameyasema Leo Tarehe 18 Mei 2024 Mwenyekiti wa jumuiya ya mitandao ya kijamii Tanzania JUMIKITA Shaban Matwebe Amesema dhima kuu ya kongamano hilo ni kujadili uandishi wa habari Kupitia mitandao ya kijamii na pamoja na upashanaji wa habari Kupitia mitandao

“Kongamano hilo litajadili mafanikio ya miaka mitatu ya serikali ya Dkt Samia suluhu Hassan ikiwa ni pamoja na maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari Duniani”.Amesema Matwebe

Amebainisha kuwa mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii na uzalendo,fursa zilizopo kwenye Tasnia hiyo

Matwebe Amesema mafanikio na changamoto Ili kutoa mchango wa kiuendeshaji Kwa wadau Kupitia JUMIKITA na mapendekezo yatakayosaidia serikali kwenye uratibu wa sera za jinsi ya kuunganisha.sayansi ya uchumi wa taifa na uchumi wa Taarifa

Aidha Matwebe Amesema kongamano hilo linatarajiwa kuwa na washiriki Zaidi ya 500 na litaongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa

/ Published posts: 1886

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram