
Na Madina Mohammed IRINGA WAMACHINGA
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Nchini (TMDA) kwa mara ya tatu leo imetoka tuzo kwa Waandishi wa habari bora wa Uandishi wa habari za dawa, vifaa tiba, vitendanishi na bidhaa za tumbaku.

Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo ambazo pia ziliambatana na Kikao kazi Cha Wahariri na Waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba, Sura 219 iliyofanyika Mkoani Iringa, Dkt.Adam Fimbo amewapongeza waandishi walioibuka washindi huku akiwasisitiza wandishi kuendelea kuandika habari za TMDA zenye kuleta tija kwa jamii.

Amesema kuwa tuzo hizo ni sehemu ya jitihada za TMDA wanazozifanya kwa waandishi wa habari katika kuripoti habari za dawa, vifaa tiba, bidhaa za tumbaku na vitendanishi katika kuuhabarisha umma wa watanzania.

โTunataka mtuandike mambo yote ambayo mmeyachunguza vizuri,yaandikwe ili tujirekebishe ,โamesema na kuongeza
โTuzo hizi ni maazimio ya kikao kazi yaliyofanyika mkoani Arusha Mwaka 2021 ambapo Mwaka 2022 tulianza utekelezaji wake,โamesema

Aidha amesema utoaji tuzo hizo ni kutambua kazi kubwa inayofanywa na waandishi wa habari katika kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya Dawa na vifaa tiba na ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza endapo dawa hizo hazitatumiwa ipasavyo.