128 views 58 secs 0 comments

KAMPUNI YA TUOCH ROAD KUANZISHA SAFARI ZA NDEGE KATI YA TANZANIA NA CHINA

In KITAIFA
May 16, 2024



Na Mwandishi Wetu Beijing

Kampuni ya  Touchroad Holding Group ya nchini China inayojihusisha  na kuziunganisha nchi za Afrika na fursa mbalimbali zilizoko nchini China hasa utalii, biashara na uwekezaji itazindua safari za ndege kati ya Tanzania na China kuanzia mwezi Juni mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini China jijini Beijing.

Amesema mpango huo utasaidia kuitangaza Tanzania katika soko la utalii la China.

Ameongeza kuwa Kampuni hiyo pia inayojihusisha na kusafirisha watalii sehemu mbalimbali Afrika , Tanzania itapata fursa ya kujitangaza kupitia vipindi vyao maalum vya Televisheni vijulikanavyo kama”Travel with Stars to Africa” na “Sisters  Extraodirnary Journey”.


Pia amesema kampuni hiyo inajipanga kuanzisha mashindano ya mbio ya marathon nchini Tanzania Bara na Zanzibar kwa lengo la kuimarisha utalii wa michezo.

Aidha, ametumia fursa hiyo kuwahamasisha wawekezaji wa China kutembelea Tanzania na kuwekeza katika maeneo ya ya vivutio vya utalii pamoja na kuunga mkono filamu ya ” Amazing Tanzania ” kwa kuitangaza katika majukwaa mbalimbali.

Mwenyekiti wa Kampuni ya Touchroad Holding Group,Dkt. He Liehui
amesema kampuni hiyo  imekuwa ikiandaa safari za makundi ya wafanyabiashara na watalii katika nchi za Afrika kwenda China na Tanzania.

Ameongeza kuwa lengo  ni kujitangaza kuwa baada ya janga la  UVICO – 19  kampuni hiyo imekuja na mipango kadhaa ikiwa ni pamoja kuandaa safari za kitalii kwa kutumia ndege za kukodi za ATCL mara moja kwa kila mwezi.

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram