

Meya mstaafu wa kata ya Ubungo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Boniface Jacob amesema katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Nchi nzima hivi karibuni wamejiandaa kushinda mitaa 48 ya jimbo la ubungo.
Boniface afunguka hayo wakati akikabidhi mifuko ya simenti na vifaa vingine vya ujenzi wa ofisi ya Chama katika kata ya Ubungo.
Aidha ameeleza kusikitishwa na wale wote wanaokichafua Chama hicho.
“Kitu pekee tunachoweza kukitendea haki Chadema ni kuhakikisha kwanza kina imarika lakini kinakuwa kikubwa zaidi,ili na wengine nao wafaidike na hiki Chama,ndio maana tukiona mtu anaharibu Chama tunamuangalia kwa jicho baya sana,mimi nimeshakuwa Meya nimekula matunda miaka mitano nimepewa gari la Prado na serikali ya CCM na mafuta bure”amesema Boniface.