318 views 2 mins 0 comments

KAMPUNI YA MERIDIAN BET KUJA NA PROMOSHENI YA TOBOA KIBINGWA

In BURUDANI
May 13, 2024

Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya Meridianbet inayoongoza kubashiri leo wazindua promosheni mpya ya “Toboa kibingwa” kwa kushirikiana na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Money huku lengo kuwapa thamani wateja wao ambapo washindi wawili katika promosheni hiyo watapewa bajaji mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo hii Meneja Mwandamizi wa huduma za malipo Tanzania Allan Rwebogara amesema kuwa wamefurahi kushirikiana na kampuni hiyo kwa kuanzisha promosheni ya kusisimua kwa wateja wao, huku akiahidi kutoa thamani na burudani kwa wateja wao.

Amesema kuwa, mteja atatakiwa kila siku kuweka shilling 25000 katika akaunt yake ya kubashiri ambapo watapata spins za bure kwenye michezo ya kasino zikiwa na fursa ya ziada ya kushinda kwa kiasi kikubwa wakati wanafurahia michezo yao pendwa ya kasino na kubashiri.

“Zawadi za wiki, washiriki wana nafasi ya kushinda zawadi za kuvutia za wiki ikiwa ni pamoja na bonasi ya asilimia 10 inayowekwa moja kwa moja kwenye akaunti zao za kubashiri”amesema  Rwebogora.

Ameongeza kuwa, washindi watatu wenye bahati watachaguliwa kila wiki kupokea simu mpya za kisasa, huku mshindi wa kilele cha promosheni hiyo kujishindia zawadi ya bajaji mpya ambayo njia ya usafiri na kuahidi kuboresha safari zao.

Kwa upande wake,Meneja wa Airtel Money Maria Mwamyalla amewahimiza wateja wa Airtel kuchukua fursa kwa kuweka pesa kwenye akaunti zao za kubashiri za Meridianbet kupitia mtandao huo.

“Wateja wa Airtel Money wanaweza kushinda zawadi hizi kwa kuweka pesa kwenye akaunti zao za kubadhiri kwa kupiga *150*60#, chagua lipia bili, kisha chagua 4 – weka namba ya kampuni, kisha andika 656565, kisha chagua ingiza akaunti id yako ya Meridian bet kama namba ya kumbukumbu ,ingiza kiasi, kisha thibitidha muamala”amesema Maria .

Aidha, amesema washindi watachaguliwa kupitia droo za kila siku  na droo kuu ya wiki itafanyika kila ijumaa na tangazo litafanyika mitandao yao ya kijamii .

Kampuni ya Meridianbet na Kampuni Airtel Money zinaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake kupitia promosheni zenye kuvutia na zawadi nyingi , Promosheni hii itaitwa “TOBOA KIBINGWA”.

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram