83 views 21 secs 0 comments

BRIGEDIA JENERALI NDAGALA AKAGUA ENEO LILILOATHIRIKA NA MAJI WILAYA YA KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM

In KITAIFA
May 10, 2024




Na Mwandishi wetu.


Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Brigedia Jenerali Hosea Ndagala tarehe  9 Mei, 2024  amefanya ziara ya kutembelea Wilaya ya Kigamboni kata ya Mjimwema Mtaa wa Maweni kwa lengo la kuangalia madhara yaliyotokea  kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam.


Awali akiwa katika kikao cha pamoja na Katibu Tawala Msaidizi (Mipango na Uratibu) Ndg. Chillah Moses katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwaajili ya kupata taarifa kuhusu hali halisi ya madhara ya mvua hizo kwa Wilaya ya Kigamboni alielezwa kuwa maeneo yaliyoathiriwa ni pamoja na Mtaa wa Maweni eneo la Bondeni  kata ya Mji Mwema pamoja na Maweni eneo la Biasi  ambayo yamezingirwa na maji  ya mvua zinazoendelea kunyesha Katika Mkoa huo.



Aidha Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu itaendelea kuratibu masuala ya menejimenti ya maafa nchini ili kuhakikisha jamii inaendelea kuwa salama na stahimilivu dhidi ya maafa.

/ Published posts: 1205

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram