179 views 4 mins 0 comments

WAMACHINGA KUPATIWA VIWANJA KUPITIA MAENDELEO BANK

In BIASHARA
May 07, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

Benki ya Mandeleo Leo imesaini mkataba wa makubaliano ya pamoja Kati yake na shirikisho la umoja wa wamachinga wa Kariakoo (KAWASSO) utakaowawezesha wafanyabiashara hao kupata viwanja vya makazi sambamba na kupata mikopo kwa ajili ya Kujengea nyumba unaojulikana kama ‘Machinga Plot Finance’.



Akizungumza na waandishi wa habari Leo May 7,2024 Mkurugenzi wa benki hiyo Dr Ibarhim Mwangalaba amesema kuwa kupitia Mkataba huo,Benki hiyo itatoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya milioni 500 kwa wamachinga karibu 500 kwa awamu ya kwanza ili kuwawezesha kumiliki viwanja hivyo.

Amesema kuwa pesa hizo zitakuwa kwa ajili ya ununuzi wa ardhi,usafishaji wa eneo husika,upimaji wa viwanja na urasimishaji ili kuwezesha mgawanyo wa viwanja kwa wanachama binafsi ili kila mnufaika aweze kuwa na hati yake.



“Mandeleo Bank PLC,tulipokea maombi kutoka Kawasso ya ujenzi wa nyumba za makazi kwa wamachinga ambapo tulikubaliana kuanza na ununuzi wa viwanja na hivyo kuwawezesha machinga wa Mkoa wa Dar Es Salaam kumiliki viwanja na hatimaye kupata makazi ya kuishi,na umoja huo tayari umeshapata hekari 89 katika Kijiji cha Magoza kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani” amesema Dr Mwangalaba na kuongeza kuwa,

Benki hiyo imeamua kuja na Mpango huo kwa kutambua changamoto zinazowakabili wajasiriamali wadogo na watu wenye makundi maalum kama la wamachinga kuwa ni ukosefu wa dhamana zinazowawezesha kupata mikopo kwa ajili ya mitaji kupitia taasisi za fedha ambapo Benki iliamua kuridhia ombi la Machinga la utoaji wa mikopo ya Nyumba kwa kuanza na viwanja.




Hata hivyo katika hatua nyingine Benki hiyo kwa kushirikiana na Kariakoo Wamachinga Association (KAWASSO) ili kufanikisha lengo Hilo la mikopo,imeingia makubaliano ya pamoja na mmiliki wa eneo husika watakapojenga wafanyabiashara hao pamoja na makubaliano mengine na kampuni ya urasimishaji ardhi ya Semsic Land Consultant Limited itakayowawezesha wamachinga Mkoa wa Dar Es Salaamย  kupata viwanja vya bei nafuu isiyozidi milioni 1 kwa kiwanja kimojaย  huku wakirejesha kidogokidogo kwa muda wa miezi 12.



Aidha Dr Mwangalaba amesema katika awamu ya pili ya mikopo hiyo, Maendeleo Bank itatoa mikopo ya ujenzi wa makazi bora kwa Wamachinga hao kupitia mikopo ya Nyumba (Housing Microfinance Loans) yenye masharti nafuu na gharama ndogo ili kumwezesha machinga kumiliki nyumba ya ndoto yake.

“kukamilika kwa Mpango huu,kutawawezesha wamachinga kumiliki ardhi na makazi bora,na pia kutawaongezea sifa ya kukopesheka zaidi ili kukuza mitaji na hii yote tunafanya kwa kuitikia kuunga mkono kwa vitendo juhudi za serikali katika kukuza uchumi na kupunguza umasikini kwa kupambania makundi maalum ikiwemo Wamachinga,vijana na wanawake kwani pia tunatoa mikopo ya Bajaj kwa vikundi ambavyo haihitaji dhamana zaidi ya Chombo chenyewe”alisema Mwangalaba



Kwa upande wake Makamo Mwenyekiti wa shirikisho la umoja wa wamachinga wa Kariakoo (KAWASO),Namoto Yusuf Namoto ameishukuru Benki ya Maendeleo kwa kutoa mikopo hiyo kwa wamachinga kwani Sasa itawawesha kumiliki viwanja na nyumba kwa ajili ya makazi.

Namoto amesema kuwa wao Kama wamachinga wameridhishwa na jinsi Benki hiyo inavyowapambania Wamachinga wa Mkoa wa Dar Es Salaam kwa kuhakikisha wanakuwa na makazi bora ya kuishi na kuwezesha kufanya biashara zao kwa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu.

/ Published posts: 1486

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram