Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amesema hatasita kubadilisha timu ya Wataalam na Mkandarasi wanaoendelea na kazi ya kurejesha mawasiliano ya barabara ya Dar es salaam- Lindi katika eneo la Nangurukuru kutokana na kasi ndogo ya kazi na usimamizi.
Bashungwa ameonesha hali hiyo ya kutoridhishwa na usimamizi na kasi ya urejeshaji wa mawasiliano katika eneo hilo na kumtaka Mtaalamu na Mkandarasi kuongeza kasi ili wamalize zoezi ndani ya muda uliotolewa.
“Mimi naweza kufukuza timu yote, bora niwaambie watanzania timu hii imefeli na niagize nyingine ambayo inaweza ikaja kufanya kazi, hatuwezi kwenda hivi”, amesema Bashungwa
Aidha, Bashungwa amemuagiza Mkurugenzi wa Matengenezo ya Barabara TANROADS kutafuta na kuongeza magari ya kubeba mawe na vifusi pamoja na mitambo ili kazi ifanyilke usiku na mchana bila kusimama.