328 views 3 mins 0 comments

BANK YA KILIMO TADB YAWEZESHA MAFUNZO YA MIKOPO KWA WATAALAMU WA KILIMO

In BIASHARA, KITAIFA
May 04, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

Benki ya  maendeleo. ya kilimo  (TADB) imetoa  mafunzo ya mikopo kwa wataalamu wa kilimo nchini ikiwa na lengo Mahususi la kuweza kuhudumia watu mbalimbali Katika huduma za kilimo huku washiriki kutoka Burundi wameweza kushiriki Katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Benki ya kilimo kwa kushirikiana na Benki mbalimbali nchini.



Hayo  yamesemwa Leo Tarehe 03 Mei 2024 jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  maendeleo  ya kilimo (TADB) Dkt  Kanaely Nnko amesema kuwa Dhumuni la kutoa mafunzo hayo ni kuweza kwenda kutoa mikopo kwenye sekta nzima ya kilimo kwani wamekuja  na wahitimu Takribani 52.  Kutoka kwenye Benki ya ushirika 20 ambazo zimeshiriki mafunzo haya.

Dkt  Nnko Amesema ni fursa kupata  washiriki kutoka nchi Jirani huku Benki ya BOT Academy.  Ambao ndio wameendesha mafunzo haya na chuo Kikuu cha kilimo SUA Sokoine university of Agriculture, Chuo kikuu cha SAUTI St Augustine University ambao wamekuwa washiriki wetu wazuri tangu Mafunzo yameanza mpaka kufikia siku ya mwisho na kuweza kuhakikisha wahitimu  wetu wa kwanza wamehitimu na vyeti.



“Tumeamua kutoa mafunzo haya  mikoani kote kutokana na wakulima waweze kupata uelewa kuhusu kilimo kimekuwa kikiendesha Mafunzo kama haya hivyo mpaka sasa mfuko wetu wa Garantii umeweza Kudhamini mikopo 270 na mikopo hiyo imetolewa na Benki la shirika hilo. Na walengwa wa kilimo. Wa moja kwa moja .tumeweza kuwafikia takribani  elfu 24”. Amesema Dkt Nnko

Kwa upande wake Makamu mkuu wa chuo kutoka chuo cha Benki ya Tanzania mkoani Mwanza  Ephurem   masanguti   Amesema sisi ni sehemu ya Benki kuu tukiwa na majukumu  makubwa ya kuweza kuelimisha Umma. Ikiwa na pamoja na mabenki. ya Fedha   pamoja na wafanyakazi wa Benki kuu  na Taaluma mbalimbali. Katika kutimiza majukumu yetu Benki kuu ya Tanzania BOT inaelimisha umma na kuchangia dira .



Aidha sisi kama Benki kuu tulipewa majukumu na Benki ya Maendeleo ya kilimo TARB ya kutengeneza  programu kwa ajili ya wakulima wadogo wadogo hususani imeenda kulenga kwenye uelimishaji wa  Mabenki na maafisa mikopo ambao wanasimamia   Benki ya kilimo katika kuweza kutoa mikopo hiyo” Amesema Makamu masanguti”.

Naye Afisa mahusiano Mollen Charles kutoka benki ya Absa Amesema kuwa Tumepata mafunzo kwa wiki mbili ya kilimo ambapo tulikuwa na mtazamo kuhudu kuwakopesha  mikopo wakulima wa chini kwani wanachangia katika uzalishaji wa  chakula.



Nae Meneja wa Mahusiano kilimo na biashara kutoka bank ya CRDB Salvatol Silvester Amebainisha kuwa mafunzo haya yamewasaidia sana kuweza kufungua mtanzamo wao Katika kukiangalia kilimo



“Kwa Muda mrefu Sasa Taasisi Nyingi za kifedha zikiwa zinaangalia kilimo Katika sehemu au sekta vya nchi ambayo zinaashiria vingi sana vya viatarishi Kwa hiyo mafunzo haya yametusaidia Katika kitufungua kuyaangalia sekta ya kilimo Katika mtanzamo tofauti Katika kuangalia fursa zilizopo Katika kilimo namna Gani kama sisi sekta binafsi tupo Katika kilimo”Amesema Silvester

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram