81 views 0 secs 0 comments

MALENGO YA RAIS SAMIA NI KUKIFANYA KILIMO KUWA NA TIJA ZAIDI

In BIASHARA, KITAIFA
May 03, 2024

JIJINI DODOMA

Wizara ya Kilimo imehitimisha bajeti yake kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 Bungeni jijini Dodoma kwa kishindo kikubwa.

Bajeti hiyo ya zaidi ya shilingi Trilioni 1.24 inatajwa kubeba matumaini ya mamilioni ya wakulima na watanzania wote kwa ujumla

Akiwasilisha bajeti hiyo, Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) amesema malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuleta mageuzi katika Sekta ya Kilimo kwa kukifanya kilimo kuwa na tija zaidi katika uzalishaji wa mazao na kupanua wigo wa ajira zenye staha pamoja na utafutaji wa masoko.

Wizara ya Kilimo imelenga kutengeneza mazingira ya wakulima kuzalisha zaidi chakula cha kutosha nchini na kulisha wengine kibiashara, hivyo Wakulima wamehimizwa kubadilika na kuishi katika falsafa hiyo.

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram