
Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Kumekuwa na Changamoto ya mfumo wa maisha Katika jamii watu wengi huwa wana matumizi ya madawa ya kulevya na wengine kuwa na msongo wa mawazo pamoja na kuongezeka kwa vitendo vya unyanyasaji na Unyanyapaaji kwa watu mbalimbali kumechangia kuongezeka kwa matatizo ya Afya ya Akili hasa kwa Vijana.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo Tarehe 02 Mei 2024 Jijini Dar es salaam Katika ukumbi wa protea hotel Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospital ya AAPH Dkt Mary Mwanyinyika Sando,amewataka wazazi na walezi wa watoto kuzidisha umakini kwa watoto ili kujiepusha wa watoto wasikumbane na matatizo ya Akili.

Aidha Dkt Sando,amesema nia ya Wazazi kuwa karibu na watoto ili kuhakikisha wanapambana na dalili za mwanzo ambazo wazazi wanaweza kuzizuia kwa mtoto wenye changomoto ya ugonjwa wa Akili.
“Tunachangamoto kubwa kwenye jamii,kweli Kuna tatizo Katika Utafiti wetu tulilenga na kuangalia nini Katika kati ya Vijana 10 15 mpaka 24 kupata matatizo ya Afya ya akili”.Amesema Sando

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa hospital ya afya ya akili Mirembe Dkt Paul Sarea amesema kwa sasa bado wazazi wanashindwa kupambana na Dalili za awali za watu wenye matatizo ya magonjwa ya akili na kupelekea kuwapeleka wagonjwa kwenye hali ya juu
Nae mtafiti Mwandamizi wa program ya Being Mental Health Initiative Kutoka Shirika lisilo la kiserikali Nchini Dkt Innocent Yusufu Africa academy for public Health AAPH Amebainisha wakati wa uzinduzi huo wa mradi wa Utafiti

Dkt Yusufu,amesema katika utafiti huo katika zaidi nchi 16 kutoka Bara la Afrika na maeneo mengi Duniani imeonesha kuongeza kwa vijana kati ya miaka 10 mpaka 24 wakiwa na matatizo Akili.
“Tumebaini mambo kadhaa yanayoweza kuchochea changamoto za Afya ya Akili Ugumu wa Maisha,utumiaji wa madawa ya kulevya,kutengwa kwa watu wenye matatizo mbalimbali na kupelekea watu kujiua.”Amesema Dkt Yusufu.

Aidha,Dkt Yusufu,amesema katika mradi huo wamebaini pia kuwepo kwa Unyanyapaa kuhusu afya ya Akili hapa nchini kutokana na Imani za Kiutamaduni kutokana na imani za kiutamaduni,uelewa mdogo katika Jamii,na upatikanaji mdogo wa huduma za afya ya akili.