122 views 14 secs 0 comments

UCHACHE WA WATU MOSHI: MWENYEKITI CHADEMA KUJIUZULU

In KITAIFA
April 30, 2024



Hii ndio hali halisi ya maandamano yaliyogonga mwamba baada ya wananchi wa Moshi kususia wito wa chama cha Demokrasia na Maendeleo, kadhia hii imepelekea aliyekuwa mgeni rasmi Ndugu Freeman Mbowe kutoshuka ndani ya gari kwa hasira akilaumu uongozi wa Mkoa kwa kushindwa kushawishi watu wengi.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kinapitia wakati mgumu katika mikutano na maandamano mbalimbali yanayoonekana kukosa ushawishi kwa wanachama na wananchi wa kawaida katika maeneo mbalimbali nchini.



Kutokana na hali iliyojitokeza Mkoani Kilimanjaro leo hii, baadhi ya wadau wa siasa wameshauri Mwenyekiti wa Chadema kujitoa katika chama hicho ili kulinda heshima yake kutokana na na aibu kubwa iliyojitokeza.

Freeman Mbowe ni mzaliwa wa Mkoa wa Kilimanjaro jambo lililodhaniwa kuwa lingewezesha kuvutia waandamanaji wengi. Hata hivyo, hali imekuwa tofauti, wachambuzi wa masuala ya siasa wameshauri mara kadhaa umuhimu wa Mbowe kuachia kiti cha Uenyekiti alichokalia kwa zaidi ya miaka 20 ili kuruhusu akili mpya na damu changa.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram