278 views 49 secs 0 comments

WIZARA YA KILIMO YAPONGEZWA KWA UHAMASISHAJI WA MATUMIZI YA MBEGU BORA

In BIASHARA
April 27, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA MOROGORO

Mkulima mmoja kutoka Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro anayefahamika kwa jina la Raha Aloyce ameipongeza na kuishukuru wizara ya Kilimo kwa jitihada endelevu katika kuhamasisha wakulima kutumia Mbegu na miche bora ili kuweza kunufaika zaidi na shughuli za kilimo wanazofanya

Katika maelezo yake, Raha ameeleza kuwa matumizi ya mbegu na miche bora yamekuwa na manufaa lukuki kama vile mazao kuweza kukabiliana na magonjwa na wadudu mbalimbali, kupata mavuno mengi lakini pia kupunguza gharaza za utunzaji wa mimea iwapo shambani

Aidha, Mkulima huyo, ametoa raia na kuhimiza wakulima wenzake kuendelea kutumia mbegu bora ili kupata manufaa hayo

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram