64 views 47 secs 0 comments

MAPINDUZI YA KILIMO YATAPATIKANA KWA KUTUMIA ZANA BORA ZA KILIMO

In BIASHARA
April 27, 2024




Na Mwandishi wetu;

Kuelekea Mei 2 & Mei 3, 2024 tarehe za Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 kusomwa na kujadiliwa Bungeni Dodoma, tumekuandalia makala fupi itakayoangazia faida atakazopata mkulima kwa kufanya kilimo kwa kutumia zana bora za Kilimo na Teknolojia ya kisasa;

1. Kutumia zana za kilimo katika uzalishaji wa mazao kutamuwezesha mkulima kufanya kazi zake kwa wakati kulingana na msimu wa uzalishaji hivyo kuongeza tija na kupunguza upotevu wa mazao kabla na baada ya kuvuna.

3. Matumizi endelevu ya mashine za uongezaji thamani mazao ya kilimo kwa kiasi kikubwa yanachangia kuongeza ubora na thamani ya mazao ya kilimo wakati wakulima wakisubiri soko zuri litakalowasaidia kurudisha gharama za uzalishaji na kupata faida kulingana na uwekezaji waliofanya

4. Matumizi ya zana bora za kilimo huwawezesha wakulima kulima maeneo makubwa kwa haraka na ufanisi zaidi hivyo kuwahi misimu mifupi ya mvua. Hii inawezesha kuzalisha mazao mengi zaidi na kumuongezea mkulima kipato na kupunguza umaskini na kupata uhakika wa chakula.

5. Matumizi endelevu ya teknolojia za kisasa na zana za kilimo hasa matrekta na zana zingine huchochea sekta binafsi kuanzisha vituo vya kutoa huduma za zana za kilimo, karakana, viwanda vidogo na kati kwa ajili ya kutoa huduma ya matengenezo, vipuri pamoja na kuunganisha matrekta madogo na makubwa hivyo kutoa fursa za kuongeza ajira kwa vijana wa mijini na vijijini.

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram