93 views 48 secs 0 comments

MAAFISA UGANI 1000 KUTOKA MIKOA 7 MBALIMBALI WAPATA VISANDUKU VYA UGANI

In BIASHARA
April 25, 2024

MAAFISA UG
Kupitia Bajeti ya kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024, Wizara ya Kilimo imefanikisha  ununuzi na usambazaji wa visanduku vya ugani 1000 kwa maafisa ugani Kilimo 1000 katika mikoa ya Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa, Ruvuma, Rukwa na Katavi, sawa na asilimia 25 ya lengo.

Kwa upande mwingine, tayari magari 46 na Pikipiki 550 kwaajili ya Maafisa ugani ngazi ya mkoa yamelipiwa na wakala wa manunuzi wa Serikali anakamilisha taratibu za manunuzi

Kuendelea kuimarika kwa huduma za ugani nchini kumewawezesha wakulima kufanya kilimo chenye tija, kuongeza uzalishaji wa mazao na kupunguza hasara ya mavuno hafifu kutokana na kufanya kilimo bila kuwa na taarifa sahihi.

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram