334 views 44 secs 0 comments

HUDUMA ZA UGANI ZAENDELEA KUIMARIKA,VISHKWAMBI 4446 VYANUNULIWA

In BIASHARA
April 25, 2024



Wizara ya Kilimo kupitia Bajeti yake ya mwaka 2023/2024 imenunua Vishkwambi 4446, kati ya hivyo vishkwambi 946 vimesambazwa na usambazaji unaendelea kwa ajili ya usajili wa wakulima, kukusanya taarifa, kuchukua alama ya nukta katika mashamba ya wakulima na utoaji huduma za ugani kwa njia ya kidijiti na kuwawezesha maafisa ugani katika ngazi ya kata kukusanya na kuingiza takwimu kwenye mfumo wa ARDS

Aidha, katika kuhakikisha wakulima wanafanya kilimo chenye tija, Wizara ya Kilimo imeanzisha kituo cha huduma za ushauri kwa Wakulima (Call centers) na kununua vifaa vya huduma za ugani katika Halmashauri 166 nchini

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram