73 views 2 mins 0 comments

RAS NGUVILA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA USIKU WA MANANE MWANANYAMALA HOSPITAL

In KITAIFA
April 24, 2024



-Akuta Madaktari waliopo kwenye mafunzo (internship doctors) katika maeneo mengi aliyotembelea

-Ajionea Daftari la msamaha (exemption) lililopo Mwananyamala kuwa na mapungufu

-Aahidi kufanya ziara Kama hizo Mara kwa Mara katika Hospitali hizo

-Asisitiza Kuwachukulia hatua wazembe wote

-Wagonjwa waelezea kuridhishwa na huduma

-Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa akiri kupokea maelekezo na kuahidi kuyafanyia kazi

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt.Toba A.Nguvila amefanya ziara ya kushtukiza Usiku wa Manane katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala ili kuona Shughuli za kutibu wagonjwa zinavyoendelea katika Hospitali hiyo

Akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Dkt. Nguvila amekuta uwepo wa Madaktari waliopo kwenye mafunzo (internship doctors) katika maeneo mengi aliyotembelea badala ya Madaktari wabobezi walioajiriwa na Serikali

Vile vile, Katibu Tawala amejionea kuwa katika Daftari la msamaha (exemption) lililopo Hospitali ya Mwananyamala yamo mapungufu katika mfumo wa utoaji wa misamaha ambapo baadhi ya wateja walibainika  kutokuwa na sifa wameonekana kutibiwa kwa njia ya msamaha hii inapelekea uwezekano wa mchepusho wa mapato ya Hospitali na Serikali kwa ujumla, misamaha inapaswa kutolewa kwa wazee, watoto chini ya miaka mitano na wajawazito

Ras Nguvila ameahidi kuendelea kufanya ziara Kama hizo Mara kwa Mara katika Hospitali za Mwananyamala, Amana, Temeke, Mloganzila, Muhimbili na  zinginezo pia kuwataka watumishi wa Afya kufanya kazi kwa weledi, Upendo na umakini mkubwa

Hata hivyo Dkt.Nguvila amesisitiza Kuwachukulia hatua wazembe wote ambao wanatumia muda wa kazi kulala usingizi, kufanya Shughuli zao mitaani huku wakiwaacha waganga pamoja na wauguzi ( intern doctors and nurses)  waliopo kwenye mafunzo kuendelea kutoa huduma wakati wa usiku

Nao wagonjwa waelezea kuridhika na huduma zinazotolewa katika Hospitali hiyo ikiwemo upatikanaji Mzuri wa Madawa na Vifaa Tiba

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dr. Mohammed Mang’una amekiri kupokea maelekezo yote yalitokewa na Katibu Tawala na kuahidi kuyafanyia kazi

*#Sekta ya Afya ni ya kumtanguliza Mungu mbele ili kila mgonjwa afurahie huduma Bora na kupata Raha ya Matibabu kwa sababu Serikali inawekeza sana katika hili#*

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram