79 views 47 secs 0 comments

MAKAMU WA RAIS PHILIP MPANGO AWASILI VIWANJA VYA JAMHURI KULIOMBEA TAIFA

In KITAIFA
April 22, 2024

Na Madina Mohammed WAMACHINGA DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewasili katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma ambapo anawaongoza Watanzania katika Dua na Maombi ya kuliombea Taifa ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na sheikh ponda katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma ambapo anawaongoza Watanzania katika Dua na Maombi ya kuliombea Taifa ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano.


Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa, ameungana na Watanzania kushiriki Siku ya Maombi na Dua ya kuliombea Taifa katika Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Tarehe 22, Aprili 2024.

Maombi hayo yanafanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali ambapo mgeni rasmi ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango.

Kauli mbiu: โ€œTumeshikamana na Tumeimarika kwa Maendeleo ya Taifa letuโ€
Mwimbaji wa injili Bahati Bukuku akiimba Katika jukwaa maalum Katika Shughuli ya Dua na maombi kuliombea Taifa 2024 Leo 22 Katika viwanja vya jamhuri Jijini dodoma
Viongozi wadini mbalimbali wakiwa Katika Dua maalum ya kuliombea taifa Katika nchi mataifa mawili ya Bara na viziwani ya siku ya muungano wa Tanzania na Zanzibar kufanyika Leo viwanja vya jamhuri Jijini dodoma
/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram