
Na Madina Mohammed DODOMA
MAKAMO wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Philip Mpango amewasisitiza Wananchi na Viongozi mbalimbali waendelee kudumisha amni iliopo katika Taifa la Tanzania ili Muungano uliopo uweze kudumu na kuyaishi maono ya Waasisi katika kudumisha amani na Mshkamano hapa Nchini.
Makamo wa Rais Dr Mpango ameyasema hayo katika Siku ya Maombi na Dua ya kuliombea Taifa mwaka huu iliofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma ambapo amesema Muungano huo imekuwa ukiimarika siku hadi siku hivyo wamekuwa mstari wa mbele kwenye kutatua changamoto pindi zitakazojitokeza.

“Muungano umezingatia misingi ya Umoja na Mshkamano hapa Nchini ambapo umeweza kuleta faida mbalimbali ikiwemo Uchumi wa Taifa kuendelea kukua licha ya changamoto zilizojitokeza katika kipindi Cha mwaka 2020”, amesema Dr Mpango.
Nae Makamo wa Rais wa pili kutoka Visiwani Zanzibar Mohammed Abdullah amesema changamoto zinazoukabili Muungano zinaendelea kutatuliwa Kwa Kasi kubwa katika kipindi Cha awamu ya sita chini ya Usinamizi wa Rais Dr Samia Suluhu Hassani Kwa kushirikina na awamu ya nane Visiwani humo.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Jenista Mhagama amewashukuru viongozi wa dini kushiriki kwenye Dua maalumu ya kuliombea Taifa la Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikwemo mradi wa Reli ya Kisasa SGR.
” Katika kuleta maendeleo Nchini Imani inatakiwa iwepo kwa kiasi kikubwa hivyo Rais wetu Dkt samia anatambua mchango wa Viongozi wa Dini zote na tunatambua kitendo hichi ni kizuri kwa nchi yetu

















