
Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM
Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya DCEA imekamata jumla ya kilogram 767.2 za dawa ya kulevya Katika mikoa ya dar es salaam,Pwani na Tanga
Hayo ameyasema Leo Tarehe 22 April 2024 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema dawa zilizokamatwa,ni Heroin kilogram 233.2, Methamphetamine kilogram 525.67 na Skanka Kilogram 8.33
“operesheni zilizofanyika DAR PWANI na Tanga zimewakamata Watuhumiwa 21 kuhusika na dawa hizo za kulevya baadhi Yao wamefikishwa mahakamani na wengine watafikishwa taratibu za kisheria zitakapokamilika”Amesema Kamishna Lyimo
Amesema Watuhumiwa waliokamatwa.wengi wapo Katika kundi la Vijana kuanzia miaka 20 Hadi 35.
Aidha Lyimo Amesema Katika mikoa hiyo Mbalimbali Iliyofanyika operesheni Kwa nyakati tofauti tofauti zimeweza kukamata dawa hizo
Amebainisha kuwa mkwajuni Tanga walikamatwa Watuhumiwa 2 za dawa za kulevya aina ya heroin kiasi Cha gramu 329.421 na wailesi Temeke zilikamatwa kilogram 1.49 aina ya Skanka na Eneo la zinga Bagamoyo zilikamatwa dawa za kulevya aina ya methamphetamine kilogram 424.84 na Watuhumiwa 3 walikamatwa na Kunduchi alikamatwa mtuhumiwa mmoja akiwa na dawa za kulevya aina ya heroin gram 158.24 pia bandari ya Dar es salaam zilikamatwa kilogram 4.72 aina ya Skanka na Watuhumiwa 3 walikamatwa na kilogram 232.69 na 100.83 aina ya Methamphetamine zulizokuwa zinaingizwa nchini Kupitia Bahari ya Hindi Watuhumiwa tisa waliokamatwa Katika tukio hili wafikishwa mahakamani