
Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM
Kampuni ya viatu ya Skechers kwa kushirikiana na Madaktari bingwa wa magonjwa yasio ya kuambukiza hususani miguu imewataka Watanzania kutumia viatu maalumu ambavyo vimetengenezwa kwa teknolojia ambayo itaasaidia kutibu magonjwa mbalimbali ya miguu

Akizungza leo Jijini Dar es salaam na Waandishi wa habari Daktari bingwa wa magonjwa yasio ya kuambukiza kutoka hospitali ya Tiba Health Care Specialized Clinic Dokta Jamil Suleiman amesema kwa muda mrefu jamii imekuwa ikisumbuliwa na changamoto ya magonjwa ya miguu hivyo viati hivyo vilivyotengenezwa kitaalamu vitasaidia kwwnye matibabu

Aidha Dokta Suleiman amesema kupitia viatu hivyo ambavyo vimeletwa na kampuni ya Skechers hapa nchini vitakua ni suluhisho kwa maradhi ya miguu kwani vimeshafanyiwa majaribio na kuweza kutibu watu mbalimbali

Kwa upande wake Meneja masoko wa Skechers Tanzania, Micky Decha amesema kampuni hiyo kwa kushirikiana na Madaktari bingwa imeamua kuja na viatu hivyo ili Kukaboliana na magonjwa ya miguu