
Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM
Mwenyekiti wa jukwaa la wanahabari wa mitandao ya kijamii Tanzania JUMIKITA Shabani Matwebe Amesema Nawashukuru watanzania kwasababu badala ya kutoa taarifa ya kuonyesha sasa tunatakiwa tuonyeshe tunachukia, tunakataa na kukemea matusi mitandaoni mapokeo yamekua ni mazuri
Hayo ameyasema Leo Tarehe 17 April 2024 Mwenyekiti wa jukwaa la wanahabari wa mitandao ya kijamii Tanzania Shaban Matwebe Amesema tuwashukuru Watanzania waliojitokeza, wengi wamejitokeza kwenye namna ya kuunga mkono kampeni ya kukataa matusi mitandaoni, kampeni ya kukataa kumdhalilisha mtoto wa kike.
“Kama ni Tanzania One ambaye ni rais anatakiwa kulindwa kwa gharama yoyote, tuna wanawake mawaziri wanatakiwa kulindwa kwa gaharama yoyote na tuna wanawake wabunge wanatakiwa kulindwa kwa gharama yoyote, tuna wanawake wapo kwenye taasisi mbalimbali wanatakiwa kulindwa kwa gharama yoyote”.Shaban Matwebe (Mwenyekiti JUMIKITA).
Lakini mwanamke pia hata kwenye familia ni kiongozi wa familia, kwa hiyo maana halisi ya kampeni hii ni kumlinda mtoto wa kike kuanzia ngazi ya juu mpaka ngazi ya chini kwenye namna ambayo tunaamini utu wake hautatwezwa-