Na Madina Mohammed
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara nchini Uturuki kwa lengo la kukuza Uhusiano wa Kidiplomasia ya kisiasa, uchumi na biashara kati ya nchi hizo mbili .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam tarehe 15 April 2024 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika. Mashariki, January Makamba amesema kuwa Rais Samia anafanya ziara hiyo kufuatia mwaliko aliyopewa na Rais wa Uturuki, Tayyip Erdogan.
“Uturuki ni moja nchi ipo kwenye kundi la nchi 20 tajiri duniani (G20), hivyo tunajua ziara hiyo itakuwa ya kimkakakti. Lengo lingine ni kupata mtaji na teknolojia ambao nchi ya Uturuki wanayo, kupata masoko ya bidhaa ambayo yapo nchini humo na kushawishi wawekezaji kuja kuwekeza nchini kwetu,” amesema Mamkamba.
Aidha waziri Makamba Amesema kuwa tayari wameshuhudia kampuni kubwa kutoka Uturuki zikifanya shughuli mbalimbali hapa nchini hatua ambayo imekuwa ikisaidia kuchochea maendeleo katika sekta mbalimbali zikiwamo za elimu, afya na maji.
Hivyo. Rais Dkt. Samia atafanya mazungumzo ya Kiserikali na Rais wa Uturuki na baadae watafanya mazungumzo ya pamoja na wajumbe wa pande zote mbili lengo likiwa ni kuangalia maeneo mapya ya ushirikiano.
Waziri makamba ameongeza kusema miaka 14 iliyopita Rais aliyekuwepo madarakani alifanya ziara nchini humo na Rais wa Uturuki alikuja nchini mwaka 2017 hivyo kuna uhusiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili.
“Tuna uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia tangu mwaka 1963 huku tukiwa tumefungua Ubalozi wetu mwaka 1979, baadae ubalozi huo ulifungwa mwaka 1984 kutokana na changamoto mbalimbali, ulifunguliwa tena mwaka 2009.
“Sisi tulikuwa na ubalozi nchini Uturuki uliofunguliwa mwaka 2017 hapo utaona kuwa uhusiano wetu ni mzuri kwa muda mrefu,” amesema Waziri Makamba.
Amesema Nchi ya Uturuki imekuwa haraka kiuchumi na ni nchi iliyopata maendeleo haraka kutokana na uhusiano na nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.