140 views 31 secs 0 comments

TMDA KUONDOA MATUMIZI YA DAWA DUNI YA BENYLIN YA WATOTO KUWA IMEISHA MUDA WAKE

In KITAIFA
April 14, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM

TMDA  imetoa taarifa Kwa umma kuwa Kuna taarifa inayosambaa Katika mitandao ya kijamii “Whatsapp”Kuhusu uwamuzi wa mamlaka za udhibiti wa dawa (national Medicine Regulator Authorities)za nchi kadhaa barani Afrika kuzuia matumizi na kuondoa (recall)Katika masoko Yao Kwa dawa duni ya maji aina ya Benylin Pediatrics syrup iliyotengenezwa mwezi Mei 2021,na kuisha Muda wake mwezi April 2024.

Dawa hiyo ya maji hutumika kuleta nafuu Kwa watoto wenye umri kati ya miaka miwili Hadi miaka 12 wanapopata dalili au magonjwa yanayotokana na hali ya mzio ( allergic condition ) kama vile kukohoa na mafua yanayosababisha homa.

Hata hivyo TMDA imeanza kufanya Uchunguzi wa dawa husika pamoja na kufuatilia taarifa hiyo Kupitia mifumo yake ya udhibiti wa dawa zinapoingia,kutuzwa,kusambazwa na kutumika nchini ambapo taarifa itatolewa mara matokeo ya Uchunguzi na ufuatiliaji utakapokamilika.

Aidha dawa hiyo iliingizwa nchini April mwaka 2022,Hata hivyo ufuatiliaji Kwa mwigizaji wa dawa hiyo nchini umebainishwa kuwa hakuna tena dawa hiyo Katika ghala lake.

TMDA inaendelea kufuatilia ubora wa matoleo mengine ya dawa hiyo na hivyo inawaelekeza wananchi kuendelea kutoa taarifa Katika ofisi za TMDA

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram