

DODOMA
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amesema katika kipindi cha miaka mitatu Serikali imefanikiwa kukamilisha viwanja vya Ndege 5 ambavyo ni Kiwanja Cha Ndege cha Geita, Mwanza, Mtwara, Songwe na Songea.
Waziri Bashungwa ameeleza hayo jijini Dodoma tarehe 5 Aprili, 2024 katika hafla ya kuangazia mafanikio ya miaka mitatu ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya Ujenzi.
Ameeleza miradi mingine ya Viwanja vya ndege vipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji ikiwemo Kiwanja Cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, Kiwanja cha Ndege cha Iringa, Kiwanja cha Ndege cha Kigoma (Awamu ya tatu), Kiwanja cha Ndege Moshi, Kiwanja cha Musoma, Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga, Kiwanja cha Ndege cha Shinyanga na Kiwanja cha Ndege cha Tabora (Awamu ya tatu).



