752 views 11 secs 0 comments

MADARAJA 8 MAKUBWA YAMEKAMILIKA MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA

In KITAIFA
April 05, 2024

DODOMA

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Sekta ya Ujenzi imefanikisha ujenzi wa madaraja makubwa 8 yakiwemo Daraja la Wami mkoani Pwani, Daraja la Tanzanite mkoani Dar es Salaam, Daraja la Gerezani mkoani Dar es Salam, Daraja la Mpwapwa mkoani Dodoma, Daraja la Kiegeya mkoani Morogoro, Daraja la Ruhuhu mkoani Ruvuma, Daraja la Kitengule mkoani Kagera na Daraja la Msingi mkoani Singida.

Waziri Bashungwa ameyasema hayo jijini Dodoma tarehe 5 Aprili, 2024 katika hafla ya kuangazia mafanikio ya miaka mitatu ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya Ujenzi.

Aidha, Madaraja matano yapo katika hatua mbalimbali za Utekelezaji ikiwemo Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) mkoani Mwanza ambao umefikia 85%, Daraja la Pangani mkoani Tanga umefikia 23%, Daraja la Mbambe mkoani Pwani umefikia 15% na Daraja la Mpiji Chini mkoani Dar es Salaam.

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram