

DODOMA
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amesema, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea na miradi mbalimbali ya kupunguza msongamano wa magari katika Miji na Majiji kwa kujenga barabara za juu (Fly Overs) kwenye Makutano ya barabara, Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo haraka (BRT).
Bashungwa ameeleza hayo jijini Dodoma katika hafla ya kuangazia Mafanikio ya Miaka Mitatu Madarakani ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ametaja majiji ambayo miradi hiyo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji ikiwemo jiji la Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Mbeya na Arusha.


