273 views 2 mins 0 comments

WAZIRI MBARAWA KICHWA MCHOMOKO KUESHIMISHA TAIFA,YALISEMWA SANA SASA YAMETIMIA

In KITAIFA
April 03, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM

Shirika la RELI la Tanzania TRC imeeka historia ya kwanza Kwa kuleta seti ya kwanza ya treni ya kisasa ya EMU,Vichwa vitano vya umeme na Mabehewa matatu ya abiria ambavyo vimewasili Katika bandari ya Dar es salaam

Serikali Kupitia shirika la RELI Tanzania imepokea jumla ya Mabehewa 65 ya abiria,vichwa 9 vya umeme na seti Moja ya EMU,seti zengine za EMU zitaendelea kuwasili kila mwezi Hadi oktoba 2024

Kuwasili Kwa vitendea kazi kunaifanya TRC kuwa tayari kuanza huduma za usafirishaji abiria Katika RELI ya kiwango Cha kimataifa



Hayo ameyasema Leo Tarehe 03 Machi 2024, waziri wa Uchukuzi prof Makame Mbarawa Amesema EMU itakuwa na seti kumi tumeagiza ambayo gharama yake itakuwa takribani Dola za kimarekani milion 190

“Kila seti Moja itakuwa inauwezo wa kuchukua gari nane(Mabehewa) na kila seti itachukua abiria 589 kwa mpigo,Kwa vile RELI yetu ya kisasa ya SGR itatumia Mabehewa au vichwa hivi vya kutoka hapa Dar es salaam, Morogoro na Dodoma hasa kwenye maeneo mafupi”.



“Yamesemwa maneno mengi watanzania wamesema mengi lakini ukweli ukidhihiri uongo unajitenga, serikali yetu inafanya mambo makubwa kila siku mulikuwa hamtuamini na wengine wameandika mambo mengi kwenye mtandao lakini ukweli Leo umejidhihirika na yapo hapa”.Amesema Prof Mbarawa

Nae Kaimu mkurugenzi mkuu wa TRC Amina Lumuli Amesema tuko kwenye kushusha seti ya kwanza ya EMU ambayo itakuwa na mabehewa nane za kubeba abiria 589 na kazi ya kushusha imeanza tarehe 1 tunategemea Leo itakamilika baada ya kukamilika tutajiandaa Kwa ajili ya Majaribio Ili kuweza kuona combability ya njia na Mabehewa yenyewe baada ya hapo basi kama TRC tukotayali kutoa huduma bola Kwa wananchi



“Kwa jumla tumeshapokea Mabehewa 65,vichwa 9 vya umeme ambavyo vyote hivyo vipo tayali kutoa huduma ya abiria baadae tutaanza kutoa huduma ya mizigo”Amesema Lumuli

Aidha Meneja wa mradi manunuzi za Treni ya Mwendokasi TRC Eng Kelvin Kimario Amesema Kuna maeneo treni inaitaji Kuna na spidi maarum Kwenye Yale maeneo Kuna njia ya kumuongoza dereva Kwa dereva aking’ang’ania kwenda spidi 160 ikifika Katika maeneo Yale treni hii itapunguza mwendo

/ Published posts: 1588

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram