
Na Mwandishi Wetu DAR ES SALAAM
Mjumbe wa Halmashauri Kuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Steven Wassira amesema hakuna haja yakuchapisha fomu ya mgombea uraisi ndani ya chama hicho kwakuwa tayari wana mgombea ambaye anatosha.
Wassira alitoa kauli hiyo wakati anahojiwa kwenye moja ya kipindi cha luninga alipoulizwa kuhusu mchakato wakumpata mgombea urais ndani ya chama utamaduni wa CCM rais anatakiwa atawale vipindi viwili hivyo rais Dk.Samia Suluhu Hassan anapaswa kugombea tena kipindi cha pili.
“Mnasema kipindi kinaisha sisi CCM hatuna tatizo kubwa,nimesikia baadhi ya wenzangu wanasema mwakani tuchape fomu moja mimi nasema tutagharamika bure kuchapa fomu ya nini,sisi tuna mgombea tayari,na sio kwa hisia kwa utamaduni.
“Utamaduni wa chama chetu ni kuwa ukimaliza kipindi cha kwanza unaelekea cha pili kwa mujibu wa sheria unakuwa mgombea,kwa hali hii hakuna mwana CCM anayesema anataka fomu na kama yupo tumwambie mwaka huu hazipo fomu,kwa sababu kama fomu tunajaza ya nini wakati mgombea yupo,”alisema Wassira.
Alisema mgombea urais wa ndani ya chama wanaenda kamati kuu na mgombea wao ambaye pia wekupiga kura ndo mwenyekiti,tunasema ndiyo,tunasema sawa tunaenda mkutano mkuu tunapiga kura tumemaliza mimi naona hakuna sababu yakutoa fumu kwa sababu wana CCM wana mgombea wao kwa mujibu wa taratibu,”alisema Wassira.
Alisema sio CCM tu vyama vingi mwaka huu wanapiga kura hata chama cha Democratic cha nchini Marekani nacho kinasimamisha mgombea wao huyo huyo aliyepo ambaye ni rais aliyepo madarakani Joe Bidden.
“Wao mgombea wao ana miaka 81 na wengine wanasema anasahau lakini wenyewe wamesema huyo huyo anayesahau atagombea.
“Huko sisi mgombea wetu hana tatizo lolote na anachapa kazi,ndo maana nasema hakuna haja yakuchapa fomu moja ya nini,maana kuchapa fomu moja ni gharama zaidi kuliko hata ukichapa fomu nyingi gharama inashuka,”alisema Wassira.
Alisema ndani ya miaka mitatu,Rais Samia amefanya mambo mengi kaondoa kero ya maji,kaboresha elimu,katekeleza miradi ya maendeleo na kwamba hakuna kata ambayo haijafikiwa na miradi.
“Tumetatua matatizo ya watu sasa naonaje kwa uchaguzi ujao naona tunaelekea kushinda tu kwa sababu tuna jambo lakuwaeleza wananchi,hoja tunazo na sababu zakutaka kuendelea kuongoza zipo na wenzetu wanaotaka kututoa nao wana za kwao tutazipeleka kwa wananchi watapima,”alisema Wassira.