
Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM
Kamati ya Bunge ya uwekezaji na mitaji ya umma imefanya Ziara ya kukagua mradi wa SGR na pia kuangalia majaribio ya TRC yanayofanywa Kwa maandarizi ya kuanza safari zao rasmi.
Mwenyekiti ya kamati ya Bunge Amesema kuwa kazi kubwa imefanyika Kwa kutoka Dar mpaka morogoro wameshuhudia kuwa serikali imefanya uwekezaji mkubwa sana na Usimamizi umekuwa wa hali ya juu
Hayo ameyasema Leo Tarehe Machi 27,2024 Katika kukagua mradi huo wa SGR Jijini Morogoro Amesema mradi ukiutizama thamani ya pesa unaonekana pesa imetumika

Aidha Amesema kama kamati wamelidhishwa.pasipokuwa na shaka kwamba huu mradi umetengenezwa Katika viwango vinavyostahili ,viwango vizuri na mradi unavutia Kwa watanzania
“Tumeelezwa mradi huu unafaida nyingi sana,kwanza Katika utekelezaji wake umeshatoa ajira za Moja Kwa moja Elfu 30 na ajira zisizokuwa za Moja Kwa moja ni laki na nusu ambazo zimewezesha kipato Zaidi ya bilioni 350

Mradi huo wa usafiri wa Treni zinaenda kufanya kupunguza Zaidi ya nusu ya safari na Muda ambao Magari huwa yanatumia kutoka Dar es salaam kutoka Morogoro na watanzania watatumia mda mfupi kusafiri na kusafirisha mizigo Yao
Ameendelea”Gharama za kusafirisha mizigo zinaenda kupungua Kwa Asilimia 40 huu ni mradi ni mkubwa sanaย na mzuri na jinsi tulivyoshuhudia Kwa maelekezo ya Rais treni hii ianze julai mwaka huu tumeona kabisa unaenda kufanikiwa”

Wanakamati wameipongeza serikali ya awamu hii ya sita Kwa kazi kubwa iliyofanyika Kwa kutoa fedha nyingi Kwa mradi huo,mradi huu ni mradi ambao umegharimu Zaidi ya pesa Trilion 23 na teali wameshatoa Asilimia 40 ya fedha
Kamati hiyo ya bunge imeweza kutoa Rai yao Kwa TRC waweze kuitunza miundombinu hiyo na waweze kuwasimamia wakandarasi wamalize kazi zilizosalia

Nae mkurugenzi mkuu wa TRC Masanja kadogosa Amesema watatekeleza maelekezo yaย Mhe Rais kabla ya mwezi julai unaanza kupeleka abiria dodoma
Amesema kila kitu kimekamilika vimebakia vitu vidogo vidogo na Bei zipo Zinashughurikiwa na watu wanaohusika kabla ya mwezi huu wa julai kila kitu kitakuwa wazi na kujulikana Kwa Muda wa safari