224 views 39 secs 0 comments

NAPE: UTULIVU ULIOPO NI MAONO YA SAMIA

In KITAIFA
March 27, 2024

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema utulivu uliopo kwenye sekta ya habari nchini umechangiwa na maono ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, kusherehekea kilele cha programu maalum ya Kurasa 365 za Mama, iliyojikita kuangazia mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Nape amekiri utulivu katika sekta ya habari na mawasiliano nchini umetokana na uvumilivu wa Rais Samia ambao unaakisi maana ya majina yake matatu.

โ€œTunazungumza kurasa 365 za mama, naangalia majina haya matatu, naangalia Samia ina maana kubwa inayotambuklika na wengi, ni kitu chenye thamani kubwa na wote mnaona mama Samia ni mtu wa thamani kubwa, la pili nikaangalila Suluhu mtu ambaye ana uwezo wa kutatua migogoro kwa amani,โ€ amesema.

Ameendelea, โ€œHassan ni mtu mwema, kwa hiyo ukichukua Samia mtu mwenye thamani kubwa, Suluhu mtu anayetatua migogoro kwa amani na Hassan mtu mwema, mara miaka mitatu hivi tukienda naye tukamaliza naye halafu tukamuongezea mingine mitano mambo yatakuwaje?โ€.

Amesema, kutokana na utashi huo wa Rais, wizara yake haina budi kufanya kazi vizuri na vyombo vya habari na kuvihakikishia kuvipa uhuru wake na kuvisimamia vema kwani maono ya Rais Samia ni wizara kuwa mlezi badala ya kuwa muwajibishaji.

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram