156 views 2 mins 0 comments

Majaliwa: Ni suala la muda tu ujenzi wa reli ya kati

In KITAIFA
March 27, 2024
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media, Joseph Kusaga, kwenye Kongamano la Kurasa 365 za Samia zenye lengo la kutangaza mafanikio ya Miaka Mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam Machi 27, 2024. Katikati ni Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Nape Nnauye na kulia ni Waziri wa Afya Ummy Mwalimu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DAR ES SALAAM: Waziri Mkuu , Kassim Majaliwa amesema mradi wa Ujenzi wa Reli ya kati mpaka sasa umeshafika maeneo yote yanayopaswa kufikiwa.

Majaliwa amesema hayo leo Machi 27, 2024 akihitimisha kampeni ya Kurasa 365 za mama katika ukumbi wa Mlimani City Dar es salaam.

Amesema, ‘tuna mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kati ambao umeshafika kwenye maeneo yote ambayo reli hiyo inatakiwa kufika, ujenzi wa reli kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro umekamilika na umeshafanyiwa majaribio mara mbili,”.

Amesema, ujenzi wa reli kutoka Morogoro mpaka Makutopora nao umekamilika kwa kiasi cha zaidi ya asilimia 96 maeneno yaliyobaki ni maboresho na viunganishi kuhakikisha kila kitu kimekamilika.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifuatilia mjadala kwenye Kongamano la Kurasa 365 za Samia zenye lengo la kutangaza mafanikio ya Miaka Mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam Machi 27, 2024. Kushoto ni Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Nape Nnauye na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media, Joseph Kusaga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
/ Published posts: 1209

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram