161 views 2 mins 0 comments

UCHUMI WA TANZANIA UMEENDELEA KUKUA WAFIKIA ASILIMIA 5.2

In KITAIFA
March 25, 2024

Na mwandishi wetu

Serikali imesema uchumi wa Tanzania umeendelea kukua Hadi kufikia Asilimia 5.2 licha ya athari ya mlipuko wa UVIKO 19 Duniani pamoja na vita kali ya urusi na ukraine

Msemaji mkuu wa serikali mobhare Matinyi ameyasema hayo Leo Machi 24,2024 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari Kuhusu mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Samia suluhu Hassan Madarakani

Amesema matatizo hayo yaliutikisa uchumi wa Tanzania ambao uliokuwa umefikia wastani wa ukuaji wa Zaidi ya Asilimia 7 na kuushusha Hadi Asilimia 4.2 mwaka 2020

Licha ya hayo Matinyi amesema kuwa Kwa Sasa ukuaji umefikia Asilimia 5.2 kutokana na Uongozi thabiti wa serikali ya awamu ya sita

“Aidha,imeendelea kuwa Katika kundi la nchi zenye uchumi wa pato la kati,ikimaanisha pato la wastani la kila mwananchi Kwa mwaka ambapo ingawa mwaka 2019 ilikuwa kiasi Cha Dola 10,80,lakini mwaka 2022 ni Dola 1,200.

“Serikali pia imeendelea kudhibiti mfumuko wa Bei ambapo Kwa Sasa ni Chini ya Asilimia 4 kiwango ambacho ni miongoni mwa kiwango bora Katika nchi za jumuiya kikanda ambazo Tanzania ni wanachama,kama jumuiya ya maendeleo kusini mwa Africa (SADC) na jumuiya ya Afrika mashariki (EAC)

Katika hatua nyingine Amesema Akiba ya fedha za kigeni imeendelea kuwa toshelezi ambapo Katika kipindi chote Cha miaka mitatu Hadi desemba 2023,nchi ilikuwa na akiba inayotosha kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi Kwa miezi 4.5 ikiwa ni kiwango Cha juu ya lengo la miezi 4

“Akiba hiyo ni sawa na Dola za kimarekani bilioni 5.4,”Amesema Matinyi Ambae pia ni mkurugenzi wa idara ya habari maelezo

Wakati huo huo, Matinyi amesema kuwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imeendelea kufanya vizuri Katika kipindi Cha miaka mitatu

Ni Kwa kufuata mwongozo wa Rais wa Kujenga uhusiano mzuri wa wafanyabiashara na kujali changamoto wakati wa kukusanya Kodi nchini

Amesema makusanyo yamefikia shilingi Trilion 24,14 Kwa mwaka 2022/24 kutoka shilingi Trilion 18,15 mwaka 2020/21 ikiwa ni ongezeko la shilingi Trilion 5.99

“Aidha,Kwa mwezi Desemba 2023 ulivunja rekodi ya ukusanyaji ya kila mwezi baada ya kufanikiwa kukusanya shilingi Trilion 3.05 licha ya kuwa wastani Kwa mwaka huu Hadi Sasa ni shilingi Trilion 2,13

“Ni vema kufahamu kwamba Hadi kufikia Machi 20,2024 TRA ilikuwa imeshakusanya kiasi Cha shilingi Trilion 19,21 ikiwa ni dalili ni kwamba itavuka kiasi Cha mwaka uliopita,”Amesema msemaji mkuu huyo

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram