137 views 39 secs 0 comments

RAIS DK MWINYI AHIMIZA KUHIFADHI QURAN NA KUFUNDISHA

In KITAIFA
March 25, 2024

Na mwandishi wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Waumini wa Dini ya kiislamu kuendelea kuhifadhi Quran Tukufu na kufundisha watoto wao kuisoma na pia wazidishe kutoa sadaka kwa watu wenye mahitaji hususani katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika fainali za 24 za Mashindano  ya Quran  Tukufu  Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al Hikma Foundation kwa kushirikisha  nchi mbalimbali 22 za Afrika na nje ya Afrika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam  tarehe 24 Machi 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amewataka Watanzania  kuendelea   kudumisha amani, umoja na mshikamano na kuzidi kupiga hatua za maendeleo nchini.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi ameipongeza Taasisi ya Al Hikma Foundation kwa kuandaa mashindano  hayo makubwa ambayo yanaitangaza Tanzania kwa kushirikisha nchi mbalimbali.

Pia ameipongeza  Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa kuyadhamini mashindano hayo kila mwaka.

Mshindi wa kwanza wa Mashindano hayo ni Ibrahim Sow wa  Ivory  Coast aliyepata shilingi milioni  27,  mshindi wa  pili  Haafith Abdulkariim Kabiito kutoka Uganda shilingi  milioni 17.2  , mshindi wa tatu Kamil Almin Swaleh  kutoka Tanzania shilingi milioni 11.6 , mshindi wa nne Kamilou Koura kutoka Togo shilingi milioni 8.1 na  mshindi wa tano Idris Nshimwe kutoka Burundi shilingi milioni 4.5

/ Published posts: 1480

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram