106 views 2 mins 0 comments

JESHI LA POLISI LIMEWAKAMATA WATUHUMIWA WANAOTUMIA KUIBA KWA KUTUMIA MAJINA YA VIONGOZI

In KITAIFA
March 22, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na kikosi kazi maalum cha kuzuia na kupambana na matumizi ya makosa ya kimtandao kimeendelea na kazi ya ufuatiliaji na kufanikiwa kwa mara nyingine kuwakamata watuhumiwa Claudian Makaranga mwenye umri wa miaka (28) mkazi wa Kawe, Kinondoni na Hongliang Yang wenye miaka (35) Mchina, mkazi wa Kigamboni, kwa tuhuma za kuingiza vifaa vya mawasiliano ya intanet nchini bila kufuata utaratibu wa kisheria vyenye jina la STARLINK KIT/DEVICE.


Hayo ameyasema Leo Tarehe 22 Machi 2024 Kamanda wa polisi Kanda maalum SACP  Jumanne Murilo Amesema Watuhumiwa hao wamekuwa wakijitangaza kuuza vifaa na kutoa huduma ya internet nchini kupitia
mtandao ya kijamii wa Instagram kwa akaunti yenye jina la STARLINK.


“Baadhi ya vifaa vilivyoingizwa nchini imebaika vilishauzwa na kutumika katika baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam kitendo ambacho ni kosa na kinyume na sheria kwani havijaidhinishwa na
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)”. Amesema Murilo

Amesema kuwa Vifaa hivyo ilivyokamatwa ni Starline Dish 12, Starlink
Router 12.


Polisi Kanda Maalum ya Dar inatoa wito kwa wananchi kuwa makini na matumizi ya vifaa vya mawasiliano, ambavyo havijaidhinishwa na mamlaka husika.


Pia amekamatwa Wilfred Werandumi mwenye miaka (44) mkazi wa Tungi, Morogoro na Abdulrahim Mwakibinga mwenye miaka (30), Mkazi wa Mwandege, Morogoro kwa tuhuma za kutumia majina ya Viongozi mbalimbali wa nchi na kutapeli watu, kwa kujifanya wanaomba michango ya harusi, misiba na matibabu.


Baadhi viongozi ambao majina yao yametumika katika utapeli huu ni Mh. Dr. Stergomena Tax,Mhe. Innocent Bashungwa, Mhe. Mohamed Nchengerwa, Mhe. Eng. Hamadi Masauni, na Katibu
Mkuu wa zamani wa CCM Daniel Chongolo.


Amekamatwa pia Salum Kingu mwenye umri wa miaka (25) mkazi wa Mbalizi, Mbeya na Loveness Silonga mwenye miaka (24) mkazi wa Mbalizi, Mbeya kwa tuhuma za kutumia akaunti ya mtandao wa kijamii wa Facebook yenye jina la
KOPA FASTER TULIA TRUST FOUNDATION na kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa watu mbalimbali kwa kudai kuwa wanatoa mikopo kwa masharti nafuu na haraka wakitumia
namba ya simu 0749704445.


Jeshi la Polisi limesema litaendelea na ufuatiliaji mkali wa tabia hizi na  watuhumiwa wote watashughulikiwa
vikali kwa mujibu wa sheria.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram