124 views 43 secs 0 comments

BASHUNGWA AWASILI WILAYANI MAFIA KWA ZIARA YA KIKAZI

In KITAIFA
March 22, 2024



Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb) amewasili wilayani Mafia mkoani Pwani kufanya ziara ya kikazi  ambapo amepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Aziza Mangosongo, leo tarehe 22 Machi 2024.

Bashungwa amepokelewa pia na Mbunge wa Mafia ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu, Omary Kipanga pamoja na viongozi wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi.

Katika ziara hiyo, Waziri Bashungwa atakagua miundombinu ya barabara ikiwa ni pamoja na Barabara ya Kilindoni – Kigamboni, barabara ya Kilindoni – Utende, Kivuko cha Kilindoni pamoja na kufanya mkutano wa hadhara Kirongwe.

/ Published posts: 1212

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram