125 views 3 mins 0 comments

WAZIRI MBARAWA:TUMEFANIKIWA KUFIKA SPIDI 150 KATIKA MAJARIBIO YA PILI YA MABEHEWA 14

In KITAIFA
March 18, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM

Shirika la RELI la Tanzania limefanya.majaribio ya pili ya treni ya mwendokasi kutoka Mabehewa 4 Hadi 14 likieleza kuwa ni mafanikio ya kufanya majaribio ya juu ya uwezo wa vichwa vya treni unaofikia kichwa kimoj kubeba Mabehewa 15


Majaribio hayo yaliyofanya safari kuazia Jijini Dar es salaam kuelekea mjini morogoro majira ya saa 4 dakika 20 na kufika mjini morogoro majira ya saa 6 na dakika 20 ambapo kiongozi WA msafara huo waziri wa Uchukuzi prof Makame Mbarawa

Akizungumza Leo Tarehe 18Machi 2024 Katika Ziara hiyo Waziri wa Uchukuzi prof Makame Mbarawa Amesema tunamshukuru Mhe RAIS SAMIA suluhu Kwa kutuwezesha na kituekea mazingira mazuri na kutupa fedha nyingi na Leo hii tumeona Tren yetu imetoka dar es salaam mpaka morogoro Kwa taratibu ya Majaribio

“Ndugu zangu haya sio majaribio ya kwanza majaribio tulianza mwezi novemba tulianza kwanza Kwa kukijaribu kichwa chenyewe tumefanya driving text tukafanya nyengine steps text na Sasa tunaenda kujaribu au kufanya majaribio Kwa Mabehewa yenyewe”.Amesema Mbarawa

Aidha Amesema majaribio ya kwanza walifunga Mabehewa manne na Leo hii tumekuja na Mabehewa 14 ambayo yenyewe yanauwezo wa kuchukua abiria 957 Kwa mpigo

Kwenye majaribio Yale wamekuja Kwa spidi 110,120, mpaka na 150 ni majaribio Ambayo yamefayika vizuri na wote ambao waliokuwa ndani ya treni wameona kwamba treni Ile inaenda vizuri

” Nimejaribu kuweka kikombe Cha chai kwenye meza hayakumwagika hata kidogo nimeweka kutoka dar es salaam mpaka morogoro kawaida ingekuwa treni ambayo tumeizoea Yale maji yote yangemwagika treni inaenda smooth Haina shida inaenda kisasa”Ameongeza Mbarawa

Nae mkuu wa mkoa wa Morogoro Adam Malima Amesema kibiashara tunaamini kwamba SGR ndio kituo Cha kwanza Kwa morogoro Kwa upande wa kibiashara,tunakituo kikubwa kilosa kituo kile tunatumaini kitakuwa kituo Cha uchumi na utalii Kwa sababu hata mikumi yenyewe,Tanapa mikumi national park wenyewe wamejipanga kuwa wateja wao watashukia kilosa

“Tumezungumza na wizara ya maliasili na utalii na watu wa ujenzi Tanroads Kwa ajili ya kukamilisha njia zile ambazo watalii watashukia pale kilosa ndani ya dakika 20,25  wapo ndani ya mbuga za wanyama”. Amesema Malima

Mkurugenzi mkuu wa shirika la RELI Tanzania TRC Masanja kadogosa Amesema Kwa kipande chetu maana maendeleo kipo Asilimia 98.98 Kwa maana ni Asilimia 99

Amesema Kwa sehemu kubwa ya ujenzi uliobakia ni kuingia bandarini na njia over pass tatu Kwa maana vingunguti, Nyerere na kwenda kinyerezi Kwa Asilimia 100 tutakuwa tumeshamaliza ujenzi,lakini ujenzi wa kuingia bandarini hautuzuii kuanza uendeshaji, bandarini ni Kwa ajili ya mizigo na Abiria haitatuzuia kufanya maelekezo ya Mhe Rais Samia suluhu ifikapo mwezi wa 7 tuwe teali tumeshaanza

Kipande Cha pili ni kutokea morogoro kwenda matukupora ya singida wapo Asilimia 96.7 na tunaendelea vizuri sana tunamalizia Katika hatua za mwisho

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram