

*Vitachimbwa visima vya ziada Zaidi ya 30 vya Bahari
*Jumla ya futi za ujazo zilizogundulika trilioni 57.54 zote ni za gesi asilia
MADINA MOHAMMED DAR ES SALAAM
Mamlaka ya udhibiti mkondo wa juu wa petroli(PURA) na Chuo Cha Bahari Dar es salaam(DMI) Leo wametiaa Saini mkataba wa hati ya mashirikiano
Hati hiyo inayohusu Mashirikiano Kwenye eneo la mafunzo Katika sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia, hati hiyo ambayo inayoweka misingi ya mashirikiano kati ya PURA na DMI

Akizungumza Katika hafla hiyo Leo Tarehe 13 Machi 2024 Mkurugenzi mkuu wa Pura Charles Sangweni Amesema Katika kuwezesha uwezeshaji wa kituo chenye isibati kitakachotoa mafunzo ya usalama na kujihami
“Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika, watanzania hulazimika kutumia takriban Dola za Marekani 7,000 kushiriki mafunzo hayo nje ya nchi kwa muda wa siku tano. Fedha hizo zinajumuisha gharama za mafunzo, usafiri wa ndege, malazi, chakula, bima ya afya n.k”.
“Kwa watanzania wanaofanya na wanaotarajia kufanya kazi maeneo ya baharini wakati wa utekelezaji wa Shughuli za mafuta na gesi asilia, miongoni mwa mafunzo yatakayotolewa ni opito,na bosieti”.Amesema Sangweni

Kuazishwa Kwa Kituo hicho Cha mafunzo nchiniย kitawezesha watanzania wengi kupata mafunzo sitahiki na kuongeza ushiriki Kwa wananchi Katika Shughuli za mafuta na gesi asilia zitakazotekelezwa maeneo ya baharini
Sangweni Amesema Kwa Sasa hapa nchini hakuna kituo chenye isibati kinachotoa mafunzo ya usalama na tahadhali kama bosieti mafunzo ambayo bila hayo hata kama mtu anaujuzi unaohitajika hawezi kuruhusiwa kufanya kazi Katika maeneo ya baharini
Pia amesema Azma ya PURA na DMI ya kuwezesha uanzishwaji wa kituo kitakachotoa mafunzo ya usalama na kujihami ni miongoni mwa hatua za makusudi ambazo zimeendelea kuchukuliwa na Serikali kuongeza ushiriki wa watanzania katika sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia nchini.
Ameongeza kuwa Miongoni mwa mafunzo yatakayotolewa ni Offshore Petroleum Industry Training Organization (OPITO) na Basic Offshore Safety Induction and Emergency Training (BOSIET).
Ameongeza kuwa Hadi kufikia Februari, 2024, jumla ya futi za ujazo trilioni 57.54 za gesi asilia zimegunduliwa. Kati ya kiasi hicho, futi za ujazo trilioni 10.406 zimegunduliwa maeneo ya nchi kavu na kina kifupi cha bahari na futi za ujazo trilioni 47.13 zimegunduliwa katika maeneo ya kina kirefu cha bahari.

Nae Mkuu wa chuo Cha Bahari Dar es salaam DMI Dr Tumaini Gurumo Amesema Tunaingia makubaliano Katika Taasisi hizi mbili Pura na Dmi Ili kuwezesha ushiriki wa karibu Zaidi na wa nguvu Zaidi Kwa watanzania Katika hii sekta ndogo ya mafuta na gesi
“Katika sekta hii ya Usalama wa Bahari yanaitaji usalama kwanza,kabla ya kuingia Katika chombo chochote Cha majini,hizi meli mbalimbali lazima upate mafunzo ya usalama,kujua NAMNA Gani utaweza kujiokoa wewe mwenyewe pale janga linapotokea pia linaweza kuhusisha NAMNA Gani unaweza kuwaokoa wengine”Amesema Gurumo
Shughuli za uchimbaji wa mafuta na gesi zinazofanyika baharini zinauhitaji mkubwa tena naweza kusema wa ziada wa juu ya mafunzo ya usalama baharini ukizingatia huko hakuna hospital”.
Amewataka Watanzania kuchangamkia fursa za uwekezaji katika shughuli za uchimbaji na utaftaji wa mafuta na gesi ilinkuongeza wigo wa ajila kwa watanzania.
Chuo kina kozi nyingi za ubaharia lakini kinajipanga kuongeza kozi hizo ili kukidhi matarajio na matamanio ya PURA.
Mwenyekiti wa Bodi ya PURA Halfani Halfani amesema taasisi zetu zinatekeleza kwa vitendo azima ya serikali ya kuongeza ushiriki wa watanzania katika shughuli za utafutaji,uchimbaji na uendelezaji wa miradi ya gesi.
Mwenyekiti wa Bodi ya DMI Kapteni Ernest Bupamba amesema shughuli za uchimbaji na utaftaji wa mafuta na gesi zinahitaji umakini mkubwa kwani uzembe wowote ukijitokeza unaweza kughalimu mradi mzima na ukizingatia kuwa miradi hiyo hutumia gharama kubwa.