
Madina Mohammed DAR ES SALAAM
Serikali Kwa kushirikiana na wadau wameweza kudhibiti ugonjwa wa Matende na Mabusha Katika Halmashauri 112 kati 119 na kubakiwa na Halmashauri 7
Halmashauri ambazo zenye maambukizi mapya ya Mabusha na Matende ni Pangani,Mafia,Kinondoni,Kilwa,Lindi Manispaa,Mtama Na Mtwara-Mikindani ambako Kuna jumla ya wakazi 1,203,359
Hapo awali maambukizi makubwa ya ugonjwa huo yalikuwa Katika Halmashauri 119 nchini ambapo watu milioni 31.2 walikuwa Katika hatari ya kupata maambukizi ya vimelea vya ugonjwa huo

Hayo ameyasema Leo Tarehe 12 Machi 2024 Waziri wa Afya Dkt Ummy Mwalimu Amesema Kwa mkoa wa Dar es salaam Mnamo mwezi Machi na Agosti Mwaka 2023, na Mwezi Februari 2024
Wizara ya Afya Kwa kushirikiana na Uongozi wa Mkoa wa Dar es salaam na Halmashauri za Manispaa ya Kigamboni, Manispaa ya Ubungo, Manispaa ya Temeke, Halmashauri ya Jiji la dar es salaam na Manispaa ya Kinondoni walifanya zoezi la tathmini ya kiwango Cha maambukizi ya ugonjwa wa Matende na Mabusha Katika Halmashauri hizo

“Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni na Manispaa ya Ubungo hazina maambukizi mapya ya ugonjwa wa Matende na Mabusha Kwa kipindi Cha miaka 6 baada ya kusitisha umezeshaji wa kingatiba Katika Halmashauri”,Amesema Ummy Mwalimu
Aidha Dkt Ummy Mwalimu Amesema Halmashauri ya Jiji la dar es salaam, Manispaa ya Temeke na kata 10 za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ambazo ni Bunju,Kawe,Kunduchi,Mabwepande,Makongo,Mbezi juu,Msasani,Mbweni,Wazo na Mikocheni Kwa Sasa hazina maambukizi mapya ya ugonjwa wa Matende na Mabusha

“Kata 10 za Manispaa ya Kinondoni ambazo ni Tandale,Kijitonyama,Mwananyamala,kigogo,mzimuni, magomeni,ndugumbi,Hananasif, Kinondoni na makumbusho Bado Zina maambukizi mapya ya ugonjwa wa Matende na Mabusha Kwa kiwango Cha Asilimia 2.3
Hata hivyo Mwalimu Amesema wizara ya Afya wanasitisha kampeni za umezeshaji wa kingatiba Kwa mkoa wa Dar es salaam ambayo hayana maambukizi mapya na Manispaa ya Temeke na kata 10 za Manispaa ya Kinondoni


