193 views 2 mins 0 comments

MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA, MAMA ONGEA NA MWANAO WAANZA NA WALEMAVU

In KITAIFA
March 11, 2024

DAR ES SALAAM

Tasisi ya Mama ongea na mwanao imesema hivi karibini wanatarajiwa kufanya tamasha kubwa la walemavu Nchi nzima na kuwapatia mahitaji yao mbalimbali ya msingi

Katika tamasha hilo wataungana na makundi mengine ikiwemo vijana, bodaboda, wajasiliamali na watakuwa na kauli mbiu isemayo “Mtonye mwenzako Mama tena”

Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema hii leo Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Stevu Nyerere amesema mama ongea na mwanao ipo tayari kuunga juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuwasaidia makundi maalumu kwenye jamii.

“Sisi.kama Taasisi tunawaahidi tutaendelea kuwashika mkondo nyinyi ni wapiga kura nchi hii, nyinyi ni watu kama watu wengine na mnahaki sawa na wengine”.

Pia Steve amesema Mama Samia amekuwa akijikita katika kusaidia Watanzania wa hali ya chini,katika kipindi cha miaka mitatu yake ya uongozi tunampongeza.

“Mama ameona tatizo la umeme na kulitaftia ufumbuzi na kujenga bwawa la mwalimu nyerere ambalo likianza kutoa huduma tutauza umeme mpaka nje ya Tanzania”.

Kwenye michezo Tanzania inafanya vizuri imeacha kuwa mtazamaji na mshiriki bali sasa imekuwa mshindani mkubwa na hata kushinda kwenye majukwaa makubwa ambapo wanamichezo wa sarakasi Ramadhani brothers na wengi wengi.

“Na sisi kutokana na jitihada za mama anazozifanya katika kuketa maendeleo katika taifa hili tukajitwika jukumu la kuwavika viatu watoto wa shule ambao hawana uwezo sasa hivi tumebakisha mikoa michache ambayo hatujaifikia…..nchi inajengwa na wananchi wenyewe mimi na wewe ndio tutaweza kuifanya Tanzania kuwa kama ulaya”.

Kwa upande wake Susan Lewis maarufu kama Mama Natasha amesema Taasisi ya Mama ongea na Mwanao inamjumuisho wa wasanii mbalimbali ambao wanalenga kutumia Taasisi hiyo kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo kusaidia vifaa vya shule vua watoto nk.

Nae Katibu wa jumuiya ya watu wenye upemavu ameipongeza Taasisi hiyo kwa kuwashurikisha mara kwa mara watu wenye ulemavu katika shughuli zake mbalimbali ikiwemo makongamano,mikutano na warsha ikiwa ni pamoja na kuwapa misaada watu wenye ulemavu.

“Wanayotafanya mama ongea na mwanao ni kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu katika adhima yake ya kuwainua watu wasiojiweza, wenye ulemavu,wajasiliamali”.



Aidha Steve Nyerere amekemea wanaharajati wanaotumia Mitandao ya kijamii kutukana viongozi wa juu Serikalini na kubeza jitihada zao na kuwasisitiza kuwa watumie hoja kupinga na si kutumia matusi katika kukosoa kwao.

/ Published posts: 1212

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram