129 views 2 mins 0 comments

ACT WAZALENDO WATISHIA KUJIONDOA KWENYE SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ZANZIBAR

In KITAIFA
March 09, 2024

DAR ES SALAAM

Chama cha ACT Wazalendo kimesema kitajiondoa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar kutokana na kutotekelezewa kwa makubaliano waliyoyaingia na serikali kabla ya kukubali kushiriki kwenye serikali hiyo.

ACT wanadai kuwa hoja zao tatu ikiwemo fidia kwa waliopata madhara katika uchaguzi 2020, kuundwa Tume ya Kijaji kuchunguza uvunjifu wa haki za binadamu kwenye uchaguzi Mkuu 2020 na Mageuzi katika mfumo wa uchaguzi zimepuuzwa



Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Machi 8,2024 Katibu Mkuu wa ACT Ado Shaibu amebainisha kuwa uamuzi huo ulifikiwa na Kikao cha Halmashauri kuu Taifa ya chama cha ACT Wazalendo kilichofanyika Machi 4, 2024 na kutoa agizo kwa Kamati ya Uongozi Taifa kukutana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani na Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi kupata muafaka wa hoja zao .



“ACT Wazalendo kujitoa kwenye Umoja wa Kitaifa sababu kutotekelezewa makubaliano yaliyoingiwa na Marehemu Maalim Seif Hamadi kwa niaba ya chama hiko na Rais Hussein Mwinyi kabla ya ACT Wazalendo kujiunga na Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwani kati ya hoja zao hakuna hata moja lililotekelezwa na tumekaa kimya kwa muda sasa tumechoka sasa tumeamua kufanya uamuzi huu” amesema Katibu Mkuu



Katika hatua nyingine chama hicho kilikaa Machi 7, 2024 na kufanya uteuzi Katibu Mkuu na Manaibu katibu Mkuu na Halmashauri Kuu iliidhinisha Ado Shaibu kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo kwa kipindi kingine cha miaka mitano



Aidha naye Mwenyekiti wa Mpya wa Chama cha ACT Wazalendo, Othmani Massoud Othmani kwa Mamlaka.aliyonayo amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Halmashauri kuu ya chama Marry Zakaria na Nani Kadika pia Naibu Mwanasheria Mkuu wa Chama Bonifasia Matunda, Katika idara ya habari Uenezi na Mahusiano ya Umma Katibu Salim Abdalah Biman Naibu wake Shangwe Mika Ayo na Idara ya Fedha Racher Kimambo na Hafidh Abdulrahmani.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram