Na mwandishi wetu DAR ES SALAAM
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limetoa vifaa vya kufanyia usafi soko la mabibo Jijini Dar es salaam Kwa lengo likiwa ni kuunga mkono wafanyabiashara wanawake wanaofanya Shughuli zao ndani ya soko hilo.
Msaada huo umetolewa na wanawake wa shirika hilo ni sehemu za shamrashamra za maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila march 8 kila mwaka.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa Kwa viongozi sokoni hapo afisa uhusiano wa shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Bi Adeline Berchimance Amesema shirika limewaunga mkono wanawake wafanyakazi kutoa vifaa vya kufanyia usafi Kwa sababu eneo hilo hutumiwa Zaidi na wanawake wengine ni miongoni mwa wafanyabiashara na wajawasiriamali Katika soko hilo.
“Tumekuja mahali hapa Ili kuwaunga mkono wanawake wenzetu wanaofanya Shughuli za biashara sokoni hapa maana ni matamanio yetu kuwaona wakiwa Katika mazingira safi na salama kwao hata kwetu sisi ambao ndio wateja wao wa kila siku”. Amesema Adeline
Adeline Amesema imekuwa ni utamaduni wa menejimenti ya shirika hilo kuwaunga wanawake mkono kila ifikapo Machi 8 kutoa msaada Kwa wahitaji Katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu na afya.
“siku kama ya Leo tuliwatembelea wagonjwa wa saratani Katika Taasisi ya ocean road Jijini Dar es salaam na kutoa vitu mbalimbali”. Ameongeza Adeline
Kwa upande wake meneja wa soko la mabibo Bw Geoffrey Mbwama Ameishukuru TTCL Kwa msaada wao wa vifaa vya kufanyia usafi akisema utasaidia kuondoa changamoto iliyokuwepo ya ukosefu wa vitendea kazi sokoni hapo.
“Hawa wanawake wa TTCL wametufanyia jambo kubwa sana na Sasa mazingira haya yatakuwa masafi kama inavyotarajiwa”. Amesema Mbwama
Ametoa wito Kwa watumiaji wa soko hilo kuendelea kudumisha usafi kila wakati Ili wananchi wanapofika kununua bidhaa wakute Kuna mazingira safi na hata wale wanaouza bidhaa wauzie sehemu iliyokuwa salama.
Hata hivyo meneja huyo ameziomba Taasisi na mashirika mengine kuiga mfano wa TTCL wa kukumbuka maeneo ya soko na kuyapa msaada.