Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM
Katibu mkuu wa umoja wa wanawake wa chama Cha Mapinduzi UWT jokate mwegelo amewataka wanawake wajitokeze Katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi Ili nchi iweze kuwa na viongozi wengi wanawake
Wanawake hao wametakiwa kushiriki Katika kugombea nafasi hizo kwenye kipindi Cha uchaguzi mdogo na mkubwa unaotarajiwa kufanyika oktoba 25 hapa nchini
Katibu huyo jokate mwegelo Amesema Katika kuelekea mwaka wa uchaguzi kuanzia mwaka huu 2024 katika uchaguzi wa serikali za Mitaa na Vijiji, UWT tutahakikisha tunahamasisha Wanawake wanajitokeza kwa wingi kugombea na kushika nafasi za Uongozi kuanzia Vitongoji, Vijiji na Mitaa.
“Lazima tukaongeze idadi ya Viongozi wanawake kwenye mitaa na vijiji, UWT tukiongozwa na Rais wa kwanza Mwanamke Dkt. Samia Suluhu Hassan , tutahakikisha ushiriki wa wanawake kwenye chaguzi hususani kugombea utaongezeka, ufike mwisho wanawake kuwa ndugu watazamaji na wasindikizaji na sio kuwapigia tu kura wanaume na katika hili kielelezo na kinara wetu ni Rais Dkt. Samia na ndio chachu ya mafanikio kwa wanawake.”Amesema Mwegelo
Aidha Jokate ameeleza kuwa Chini ya Mwenyekiti wetu Mama Mary Chatanda (MCC) tutahakikisha mwanamke akigombea atapitishwa na Chama na tutampambania ashinde, UWT inasema mwanamke usijione mnyingo na usijione upo peke yako, Jeshi la Mama Samia UWT litakushika mkono kila hatua.
“RAIS Samia ni msikivu, mvumilivu na anapenda kuona akina mama wanapata fursa na hatutakiwi kukatishana tamaa lazima tuungane na kutiana moyo.”
“Viongozi wengi wanapokuwa wanawake matokeo huonekana na takwimu zinaonesha akina mama ni viongozi bora.”
Wakati huo huo amewataka wanawake wajitokeze Katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Machi 8 hivyo siku hiyo ni njia mojawapo ya kupeana motisha Katika masuala mbalimbali.
Amesema siku hiyo inawapa fursa wanawake kwenye kupata uelewa wa hamasa Katika masuala mbalimbali ya kijamii
Katibu jokate amewataka makatibu wote waliopo wilayani wahakikishe wanahamasisha wanawake Katika kujiunga na umoja huo sambamba na kujisajili kwenye mfumo wa chama Cha Mapinduzi kidigitali Ili waendane na Mabadiliko ya kiteknolojia
Amesema wakijiunga na umoja huo Kupitia mfumo kidigitali watapata fursa mbalimbali
Ikumbukwe kuwa UWT ndio chombo kinachowaongoza wanawake Katika masuala mbalimbali ikiwa ni sehemu inayozingatia masuala ya kijamii na kiuchumi.