148 views 52 secs 0 comments

MHANDISI BESTA:DUNIA INABADILIKA NA TUNAPOELEKEA RASILIMALI ZINAZIDI KUADIMIKA

In KITAIFA
March 04, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM

Taasisi ya wahandisi Tanzania Kwa kushirikiana na bodi ya usajili wa wahandisi Tanzania (ERB) na chama Cha wahandisi washauri Tanzania (ACET) wameadhimisha Leo siku ya Uhandisi Duniani Jijini Dar es salaam

Mtendaji mkuu wa Tanroads Mhandisi Mohammed Besta Amesema matukio.kama haya hutunza kumbukumbu ya Yale yanayojili na kupelekea chachu ya kuondoa dhana ya kupenda kufanya kazi Kwa mazoea



Ameyasema hayo Leo Tarehe 04,Machi 2024 Katika ukumbi wa protea Jijini Dar es salaam Mtendaji mkuu wa Tanroads Mhandisi Mohammed Besta Amesema Dunia inabadilika na tunakoelekea rasilimali zinazidi kuadimika

“Kuadimika Kwa rasilimali Kuna athari kadhaa ikiwemo kuongezeka Kwa gharama za ujenzi,Lakini rasilimali zikiisha,namba pekee ya kuendelea kufanya kazi ni kuwa na ubunifu wa kutafuta rasilimali mbadala”.Amesema Besta



Amesema kuwa Nishati ya umeme wa maji na mafuta zimekuwa hadimu na kupelekea kuongezeka Kwa gharama Kwa sababu ya kuongezeka Kwa matumizi yanayochangiwa na kuongezeka Kwa Shughuli za binadamu na ongezeko la watu

“Bila ubunifu ambao unawezekana Kwa kufanya tafiti,Dunia isingekuwa sehemu nzuri za kukaa kwani Sasa tunashuhudia matumizi ya umeme wa jua,Hivi karibuni tumesikia kuwa,huko nchini Malawi Kuna kijana amebuni umeme wa hewa”,Ameongeza Besta



Aidha ametoa ushauri Katika sekta ya ujenzi ifanye kazi Kwa kushirikiana,Kwa sababu mara nyingi suluhisho za matatizo mengi Katika jamii yetu zinagunduliwa na wahandisi na mafundi ambao wana practice, Kwa vyuo vikuu.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram