496 views 4 mins 0 comments

DKT ANANILEA NKYA AWAPONGEZA ACT WAZALENDO KULIPA UZITO USAWA LA KIJINSIA

In KITAIFA
March 02, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM

Mwenyekiti wa Jukwaa la katiba JUKATA Ambaye pia ni mwanaharakati wa maswala ya kijinsia Dkt Ananilea Nkya amekipongeza Chama cha ACT-Wazalendo kwa kulipa uzito swala la kijinsia na kuamua kutengeneza sera ya jinsia ya chama 2024.

Sera hiyo inalenga kuimarisha usawa wa kijinsia ndani ya chama na kwenye ngazi mbalimbali za maamuzi ikiwa ni pamoja na kuongeza ushiriki wa wanawake,wanaume,vijana na watu wenye ulemavu kwenye maswala ya siasa,uongozi na vyombo mbalimbali vha maamuzi.

Dkt Ananilea Ametoa pongezi hizo katika Mkutano Mkuu mkuu wa Ngome ya Wanawake ACT-Wazalendo ambao umeketiwa leo Jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Hakainde Haichelema ulipo Ofisini kwao magomeni ambapo watawachagua viongozi wa ngome hiyo Kitaifa pia kupitia jukwaa hilo Sera ya Chama 2024 imezinduliwa.

Akizungumza Dkt Ananilea Nkya Amekitaka chama kuifanyia kazi sera hiyo na si kuiweka kwenye makabati ili kuweza kufikia malengo yaliyokusidiwa na kuweza kuzalisha viongozi wali bora watakao litumikia Taifa kwa uaminifuna uadilifu mkubwa.

“Sera hii itakifanya Chama cha ACT-Wazalendo kuwa cha tofauti”.Tunataka wanawake wawe kwenye nafasi za uongozi ili waweze kubadilisha Taifa”

“Vyama vingine vina la kujifunza kutoka chama Cha ACT Wazalendo na kama mkiitumia sera ya Jinsia ipasavyo ACT Wazalendo itafanya makubwa” Amesema Dkt Ananilea na kusisitiza kuwa

“Taifa lolote litakalo mwacha mwanamke/mwanaume nyuma halitakaa liendelee kamwe litabaki kuwa masikini maisha yake yote”

Pia Amewataka kuwapa kipaumbele wanawake wenye uwezo ” msiwape nafasi wanawake kwasababu tu anavaa sketi,kiongozi makini na bora hatoi rushwa anaefanya hivyo hana maono ya kuboresha maisha ya watu wala ya chama”.

Katika hatua nyingine Ameishauri Serikali kufuta viti maalumu Bungeni ili wanawake wapewe nafasi ya kugombea katika majimbo na kuweza kuingia bungeni kwa usawa kulingana na uwezo wao na si kupewa nafasi za viti maalumu ambazo zitanaongeza gharama kwa Taifa.

“Tunaweza kuzifanya kila wilaya ikawa jimbo tukaweka wagombea wawili mwanaume na mwanamke wakapimwa kwa hoja na uwezo wao kisha wakachaguliwa na kuingia bungeni kutetea maslai ya wananchi wake, tunataka usawa wa kijinsia usio wa kupendelea upande wowote”.

Kwa upande wake Mwenyekiti Ngome ya Wanawake ACT-Wazalendo ambaye anamaliza muda wake amesema wanawake wa ACT wapo tayari kushirikiana na vyama vingine katika kuleta mapinduzi ya kisiasa na kumkomboa mwanamke kiuchumi na kisiasa.


“Tupo tayari kuwakaribiaha vyama vingnine ili kuleta mapinduzi na kuweza kumkomboa mwanamke,nakishukuru Chama kwa ushirikiano waliotunyesha na jinsi wanavyotupa kipaumbele wanawake katika nyanya mbalimbali za kisiasa”.

Aidha Amewataka wanaweke hao kufanyakazi kwa kushirikiana ili kufikia malengo yao,”tunategemea kuona idadi ya wagombea kwa wanawake kuongezeka kwa zaidi ya asilimia 85 katika uchagu wa Serikali za mtaa 2024 na uchaguzi mkuu mwakani 2025″.

Nae Makamu Mwenyekiti Bara Bi Dorothy Semu Amewapongeza Wanawake wa ACT-wazalendo ppakwa ushiriki wao katika maswala ya kukuza na kukiendeleza chama ambapo kupitia juhudi zao wameweza kukikuza chama hicho kufanikiwa katika maswala mbalimbali ikiwemo kujenga ofisi ya makao makuu.


“ACT inamtambua mwanamke kama nguzo katika kufikia maendeleo katika jamii”. Amesema Bi Dorothy.

Aidha Bi semu amesema kutokana na jitihada za wanawake Chama kimeona kuna umuhimu wa kuwa na sera ya jinsia itakayoimarisha na kukuza mazingira rafiki kwa wanawake,wanaume,vijana na watu wenye ulemavu kushiriki kikamlifu katika siasa,uongozi na vyombo vya maamuzi ndani ya chama,katika vyombo vya seriakli na majukwaa mengine ya kimataifa ili kuenzi jitahada zao.

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram