229 views 3 mins 0 comments

NHIF WABORESHA KITITA CHA MAFAO KWA WANACHAMA WAO

In BIASHARA, KITAIFA
February 28, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM

Mfuko wa Bima wa Taifa wa NHIF imefanya maboresho ya kitita cha mafao kwa wanachama wake ambayo utekelezaji wake utaanza rasmi Machi Mosi mwaka 2024 ikiwa lengo ni upatikanaji wa huduma bora wa wanachama pamoja na kuongeza huduma ambazo hazikuepo hapo awali.

Aidha, amesema kuwa,  maboresho hayo ya orodha ya huduma za matibabu ambazo zinatolewa kwa wanufaika wa NHIF na bei zake ambazo hutumika wakati wa malipo kwa madai ya watoa huduma za matibabu yamezingatia maendeleo ya teknolojia na hali halisi ya bei katika soko pia kuwianisha kitita cha mafao na miongozo ya tiba iliyoboreshwa Ili kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa Kwa wanufaika wa mfuko.

Sambamba na hayo, amefafanua kuwa maeneo yaliofanyiwa mapitio na maboresho ya kitita cha mafao ni pamoja na ada ya usajili na kupata ushauri wa daktari, huduma za dawa, vipimo, upasuaji na gharama za kliniki za kawaida na kibingwa.

Amesema, Kitita cha Mafao ni orodha ya huduma za matibabu ambazo zinatolewa kwa wanufaika wa NHIF na bei zake nchini.

Konga amefafanua kuwa,maboresho ya mwisho ya Kitita cha Mafao kinachotumika sasa yalifanyika Juni, 2016.



โ€œNi takribani miaka nane sasa,hivyo kuwepo umuhimu wa kufanya marejeo yake kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuboresha upatikanaji wa huduma bora kwa wanachama na kuongeza huduma ambazo hazikuwepo.โ€

Amesema, miongoni mwa manufaa ya kitita ni pamoja na wanachama wanaotumia dawa za shinikizo la damu na sukari sasa wanaweza kupata dawa ngazi za chini.

Pia, Konga amefafanua kuwa,wanachama wanaopata huduma ya uchujaji damu gharama imeshushwa chini.

โ€œNa huduma za kibingwa na bingwa bobezi kama matibabu ya moyo, saratani, figo zitapatikana kwenye ngazi za kanda pia na sio lazima mwanachama aende mpaka hospitali za ngazi taifa,โ€amesema Konga.

Vilevile amebainisha kuwa, dawa mpya zaidi 247 zimeongezwa kwenye kitita, hivyo changamoto ya kukosa dawa kituoni imeondolewa.

Ameongeza “Gharama za vipimo 311 na upasuaji zimefanyiwa mapitio kwa kuzingatia bei za soko katika ununuzi wa vifaa na vitendanishi, gharama za uendeshaji na wastani wa faida hii itaondoa changamoto ya kukosekana Huduma za vipimo na upasuaji kutokana na changamoto ya bei”

Hata hivyo, amewaomba wananchi kuendelea kujiunga kutumia na mfuko huo kwani lengo la Serikali ni kutoa huduma za Afya kuanzia ngazi ya Zahanati, hadi Hospital ngazi ya Taifa.

Aidha, amesema mfuko huo utaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau na itaendelea kuwajulisha pindi maboresho yoyote yatakapotokea Ili kuwa na ufanisi katika utoaji wa huduma huku akiwataka wanachama na watoa huduma watakao pata changamoto wakati wa kutoa huduma kuwasiliana na mfuko huo kupitia kituo cha huduma Kwa wateja 199 bure.

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram