SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) hii leo,limezindua rasmi Treni ya umeme ya Abiria kutoka Stesheni Jijini Dar es salaam kuelekea Mkoani Morogoro.
Safari hiyo ilianza mnamo mida ya saa nne na Nusu na kuwasili Mkoani Morogoro mida ya saa sita na nusu.
Shirika la reli Tanzania TRC limeanza kufanya majaribio ya uendeshwaji wa Treni za mwendokasi kutoka Dar es salaam hadi mkoani morogoro. Kwa kiwango cha kimataifa cha SGR ukiwa ni hatua za awali ambazo zinafanyika kutoka kwenye vichwa vya treni na mabehewa.
Akizungumza mara baada ya majaribio hayo mkurugenzi mtendaji wa shirika la reli Tanzania TRC. Masanja kadogosa amesema kuwa jumla ya mabehewa kumi na moja ya kitaalamu ambayo yamefanyiwa majaribio yataenda kutumika kwa njia ya umeme kwenda kurahisisha usafiri kwa wananchi wanaoenda mkoa wa morogoro wataweza kutumia mida mchache kwenye usafiri huo wa treni .
“Majaribio haya yanafanyika. Mara baada kadhaa. Ambapo umeme utatumika ili.kuweza kujiridhisha. Juu ya ufanisi. Ambavyo vitaweza kutumika.kwenye usafiri wa abiria na mizigo kwa ujumla Huku huduma hizo zikiwa zinatolewa kwa wakati sahihi na kwenda kuwawezesha wafanyabiashara wanaosafirisha mizigo kutoka dar es salaam hadi kufika morogoro kuweza kupata mizigo kwa wakati hivyo tumeweza kufanikisha suala ambalo wananchi walikua wanasubiri kwa muda mrefu
.
Tunatarajia kupokea vichwa vitano na seti nyingine ya kwanza Treni ya kisasa ya EMU (Electric. Mutiple Unity). Huku mwishoni Mwa mwezi March mwaka huu shirika litaweza kufanya majaribio. Kwa kifaa ambacho kitawasili nchini.ili kuweza kuweka usalama. Wa abiria kabla ya kuanza kutumia vifaa hivyo.
Aidha mkurugenzi kadogosa ameongeza kuwa maendeleo ya mradi wa SGR yameweza kufikia aslimia 98.84 kutoka kwenye kipande cha Dar es saalam hadi kufika mkoani morogoro. Km 300. Ikiwa ni asilimia 96.35 kutoka kipande cha morogoro_Makotupora asilimia13.86 huku kipande cha Tabora isaka asilimia kipande cha 52.60 huku kutoka mkoani Mwanza_ isaka. “amesema mkurugenzi kadogosa”
Kwa upande wake mkazi wa Morogoro Saidi nasoro amesema tunaishukuru serikali ya Dkt samia suluhu hasani kwa kuweza kutulea treni ta kisasa mkoani kwetu morogoro kwani treni hiyo itaenda kuleta matunda kwa wafanyabishara kwani wasafiri kutoka kwenye kituo hicho watanunua bidhaa kwenye maeneo hayo ya kituo cha treni hiyo.
Tumeweza kujipatia Ajira kutokana na mradi huo kwani tulikua tunafanya kazi ndogo ndogo Katika kukamilisha mradi huo NA hivi karibuni kituo cha mabasi ya abiria kinaenda kujengwa hapa ili kuondoa usumbufu wa baadhi ya abiria wanaoshuka kwenye kituo hicho NA kwenda kuelekea kwenye shughuli zao hivyo nitoe pongezi kwa viongozi wote ambao wameweza kufanikisha mradi huu kufika mkoani kwetu morogoro.
Aidha amewatoa wasiwasi Watanzania wanaodhania kuwa umeme ukikatika utaweza kuleta athari kwa Treni hizo kuwa sio kweli umeme wake umeunganishwa kutoka grid ya taifa hivyo si rahisi umeme kukatika kwenye njia ya Treni.
Ameongeza kuwa katika majaribio hayo walimeambatana pamoja na Msemaji wa Serikali,wasanii, waandishi wa habari,wahariri na baadhi ya wafanyakazi wa TRC.
Treni hiyo inauwezo wa kutembea Km/h100-160.