147 views 2 mins 0 comments

TPA YASAINI MKATABA WA KUHIFADHI NA KUSAMBAZA BIDHAA ZA MAFUTA KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM

In BIASHARA, KITAIFA
February 26, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM

Mamlaka ya Usimamizi wa bandariย  Tanzania TPA imeingia mkataba wa ujenzi wa matenki na Miundombinu ya kupokelea,kuhifadhi na Usambazaji wa bidhaa ya mafuta Katika bandari ya Dar es salaam

Waziri wa uchukuzi Mhe prof Makame Mbarawa ameshuhudia utiaji Saini wa mkataba huo wa matenki 15 utakaogharimu shiringi bilioni 678 mpaka kukamilika kwake na unatarajia kukamilika Katika kipindi Cha miezi 24

Akizungumza Katika hafla hiyo ya utiaji Saini mkataba huo, tarehe 26 frebuari 2024 waziri wa uchukuzi Mhe prof Makame Mbarawa Amesema mradi huo utakuwa na manufaa sio tu Kwa Tanzania,Bali Kwa nchi nyingine zinazotegemea bandari ya Dar es salaam Katika kupokea bidhaa za mafuta

“Tuhakikishe kwamba mkandarasi anasimamiwa ipasavyo Ili aweze kukamilisha mradi huu ndani ya wakati na kuhakikisha kwamba thamani ya pesa ya mradi huu unapatikana, kama mradi nilivyosema ni miaka 2 tunataka mradi huu wa matenki umalizike Kwa miaka 2 kama mkataba ulivyosema”. Amesema mbarawa

Aidha Mbarawa Amesema Kuanza maandalizi ya kupata vitendea kazi Kwa watumishi wenye weredi wa kutosha wakutoa huduma Katika eneo la bandari hasa Katika eneo la haya matenki

“Tusisubili mpaka tunakabidhiwa mradi ndo tunatafuta wafanyakazi Sasa hivi tuanze kujipanga tutafute Vijana wenye uwezo tuwape elimu Ili baada ya siku wakafanye kazi hiyo ya kuhudumia matenki haya Kwa uwadilifu mkubwa na weredi mkubwa”. Ameongeza Mbarawa

Kwa upande wake mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya Usimamizi wa bandari Tanzania TPA Bw Plasduce mkeli mbosa Amesema upotevu wa mafuta Kwa Sasa ni Asilimia Moja ambapo kiwango kinachotakiwa ni Asilimia 0.25 hivyo ujenzi wa matenki hayo utapunguza upotevu huo

/ Published posts: 1209

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram